ANAYEKUMBUKWA: EMMANUEL GABRIEL MWAKYUSA YANGA HAWAKUPUMUA
Na Prince Hoza, DAR ES SALAAM
MIAKA ya mwishoni na 90 na mwanzoni na 2000 alitokea mtu mmoja hatari sana Emmanuel Gabriel Mwakyusa aliyekuja kutikisa katika klabu ya Simba.
Gabriel alitamba na klabu hiyo na akatokea kuwa mmoja kati ya qashambuliaji hatari kabisa kuwahi kutokea, pia akatamba na timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars.
Gabriel alisajiliwa na Simba sambamba na mshambuliaji mwenzake Godfrey Mhando lakini wakati huo Mhando alikuwa katika ubora wa hali ya juu.
Alipotua Simba Gabriel alitokea kuwa shujaa na kumfunika kabisa Mhando waliotokea wote Nathareth ya Njombe, Gabriel alifanikiwa kutikisa kwa mabao yake na kuitungua Yanga mara tano.
Watu wa Yanga wanamwogopa sana mshambuliaji huyo aliyepata pia kuzichezea Mtibwa Sugar, Prisons na Rayon FC ya Rwanda, Gabriel aliyezaliwa Mei 21, 1984, alikuwemo kwenye kikosi cha heshima cha Simba kilichoweka rekodi mwaka 2003.
Simba mwaka huo iliingia hatua ya makundi Ligi ya mabingwa barani Afrika tena ikiitoa mashindanoni na kuivua ubingwa wa Afrika Zamalek ya Misri.
Simba ilitangulia kuifunga Zamalek wakati ikiwa katika ubora wake bao 1-0 Uwanja wa Taifa Dar es Salaam (Sasa Uhuru), na katika mchezo wa marudiano Simba ikafungwa 1-0 mjini Cairo Misri na kufanya matokeo yasomeke 1-1 na baadaye kupigiana penalti tano tano Simba ikashinda kwa penalti 4-3 na kuvuka kwenye makundi