KOCHA MPYA SIMBA ATUA KUSAINI MKATABA
Na Prince Hoza
KOCHA mpya wa klabu ya Simba Mcameroon Joseph Maurus Omog anatarajia kuwasili Alhamisi tayari kabisa kusaini mkataba wa kuinoa timu hiyo msimu ujao.
Omog ambaye aliwahi kuzinoa Leopards ya DRC na Azam FC ya Tanzania zote akiziwezesha kupata ubingwa wa nchi, anataraji kuiongoza Simba kwa ajili ya msimu ujao na huenda akasaini mkataba wa miaka miwili.
Habari ambazo Mambo Uwanjani inazo zinasema kuwa Omog atakuwa kocha mkuu ndiye atakayependekeza usajili wa wachezaji wa kimataifa, Omog alizaliwa Novemba 30, 1971 Cameroon na amekuwa kocha nwenye mafanikio.
Msimu ujao Simba ishindwe yenyewe kutwaa ubingwa wa bara kutokana na bahati aliyokuwa nayo na uwezo pia, kikosi cha Simba kinasukwa upya huku Jackson Mayanja akitajwa kuwa msaidizi wake