BEKI MPYA YANGA AULA CAF
Na Mrisho Hassan DAR ES SALAAM
BEKI mpya wa upande wa kushoto wa mabingwa wa Ligi kuu bara na kombe la FA, Yanga SC, Hassan Ramadhan Kessy ameula baada ya kocha mkuu wa mabingwa hao Mholanzi Hans Van der Pluijm kumwidhinisha katika usajili mpya CAF.
Yanga inatakiwa kufanya usajili wa nyongeza hasa baada ya kufaulu kucheza hatua ya makundi kombe la Shirikisho barani Afrika, kwa kufanikiwa hatua hiyo Shirikisho la soka Afrika CAF inazitaka timu zote zilizotinga hatua hiyo kusajili upya.
Yanga sasa itasajili wachezaji wengine wawili au watano na tayari kocha wa mabingwa hao Hans Pluijm amependekeza majina ya nyota wawili wapya Hassan Kessy aliyesajiliwa kutoka Simba na Juma Mahadhi aliyetokea Coastal Union.