MANJI ACHUKUA FOMU YANGA, AWAVUA UANACHAMA WALIOCHUKULIA FOMU TFF
Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
MWENYEKITI ya Yanga Yusuf Mehbood Manji leo ameamua kuchukua fomu ya kuwania tena nafasi yake ya uenyekiti katika makao makuu ya klabu hiyo Jangwani.
Manji pia ametumia fulsa hiyo kuwavua uanachama wale waliokwenda kuchukulia fomu za kuwania uongozi makao makuu ya Shirikisho la mpira wa miguu TFF.
Yanga leo imeanza mchakato wa kufanya uchaguzi wao mkuu unaotarajia kufanyika Juni 11, wakati ule uliohitishwa na TFF utafanyika Juni 25.
Wakati huo huo Manji akitumia wadhifa wake amemvua uanachama aliyekuwa mwenyekiti wa matawi ya Yanga mkoani Dar es Salaam Mohamed Msumi na kuwasimamisha wengine wote waliodiriki kuchukulia fomu zao za kuwania uongozi TFF