MAONI: SIMBA WEKENI MAMBO HADHARANI, USAJILI WA KIMYA KIMYA MAANA YAKE NINI

Na Prince Hoza, DAR ES SALAAM

NIMEMSIKIA mwenyewe mwenyekiti wa kamati ya usajili klabu ya Simba Kapteni mstaafu wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) Zacharia Hanspoppe akisema kwamba Simba itafanya usajili wake kimya kimya.

Maneno hayo si kwamba yamenikera mimi peke yangu hapana, wapo mashabiki wa Simba wameniandikia meseji kwamba hawafurahishwi na Hanspoppe  mashabiki hao wanataka bosi huyo wa usajili ajiweke kando ili awapishe wengine.

Usajili wa kimya kwa sasa hauna maana yoyote ikiwa mchezo wa mpira unachezwa hadharani, hakuna faida yoyote ya kufanya usajili kwa kuogopa wenzako wanafanya nini.

Hivyo namuomba Hanspoppe aachane na maneno hayo na awasajilie majembe Wanasimba ili wasuuzike na mioyo yao, Tetesi za usajili zimeanza kuenea kuwa Sinba wamemsajili kiungo wa Yanga Salum Telela.

Mbali na Telela pia Simba inatajwa kukamilisha dili ya kumchukua mshambuliaji wa Ndanda FC ya Mtwara Atupele Green, Hanspoppe kutuambia usajili utakuwa wa kimya kimya anamaanisha nini! Paul Kiongera (Pichani) amesajiliwa na Simba akitokea KCB ya Kenya lakini hatuzioni cheche zake.

Mshambuliaji huyo alisajiliwa mwishoni mwa kufungwa kwa dirisha la usajili, kusajili kimya kimya hakuna faida ikiwa Yanga wanawasajili wachezaji wote wanaoaminika kuwa ni wazuri, Yanga tayari wamewasajili Hassan Kessy, Benno Kakolanya, Vincent Andrew "Dante" na wengineo.

Usajili huo umeonekana kuwashtua Simba kwani tayari baadhi ya wachezaji waliosajili Yanga walikuwa wakipigiwa hesabu za kutua Simba, Lakini ukimya wa viongozi wa Simba ukasababisha nyota hao kusainishwa Yanga.

Wakati dirisha la usajili likitazaniwa kufunguliwa kesho kutwa, mabosi wa kamati ya usajili wanasema hadharani kwamba watasajili kimya kimya, ina maana mambo yao hayatakuwa hewani.

Huo sasa ni usajili wa magumashi maana mashabiki hawataweza kujua hatma ya timu yao msimu ujao, Lakini kuna fununu nyingi tu ambazo mashabiki walitakiwa kuzifahamu mapema.

Usajili wa kimya kimya una faida na hasara, faida yake ni kumsajili mchezaji mzuri ambapo wapinzani wako hawamjui, Mambo ya fedha nayo yanahusika katika zoezi hili la usajili.

Kwa mfano Simba inataka kumchukua Salum Telela halafu wanataka kumpa milioni 20 lakini Azam au Mwadui wakampandia dau na kumalizana nao, Hanspoppe anatakiwa kuweka mambo hadharani ili Wanasimba wafurahie timu yao

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA