YANGA YATUA UTURUKI TAYARI KUWAVAA WAALGERIA

Na Ikram Khamees, Antaria, UTURUKI

Mabingwa wa soka wa Tanzania bara Yanga SC wamewasili salama nchini Uturuki na wataendelea na mazoezi yao kwa ajili ya maandalizi yao ya michuano ya kombe la Shirikisho barani Afrika.

Yanga imefikia katika mji wa Antaria ambapo mazingira yake yanafanana kabisa na Algeria, mabingwa hao wa bara mara 26 watacheza na wenyeji wao MO Bejaia kabla hawaelekea Dar es Salaam kuwapokea TP Mazembe ya DRC.

Ziara ya Uturuki itatumika kama sehemu ya maandalizi yao, Yanga imesafiri na wachezaji wake 21 huku wengine wakiachwa Dar es Salaam, mmoja kati ya wachezaji waliotua hapa Uturuki ni beki wa zamani wa Simba Hassan Kessy ambaye muda wote alionekana mwenye furaha

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA