BEKI WA MTIBWA SUGAR AUAWA DAR
Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
Matukio ya kinyama yanazidi kuongezeka kila kukicha hapa nchini na safari hii mchezaji wa zamani wa Toto Africans, Mtibwa Sugar, Azam FC na Vijana ya Ilala John Mabula amefariki dunia baada ya kuuawa kwa kuchomwa kisu.
Kiungo wa zamani wa Yanga SC na Mlandege ya Zanzibar Deo Lucas ameitonya Mambo Uwanjani kuwa marehemu alikutwa na mauti akiwa na shemeji yake maeneo ya Kitunda Dar es Salaam.
Deo anasema, Mabula akiwa anamsindikiza shemeji yake wakakuta kuna ugomvi njiani ambapo muda si mrefu wakavamiwa wote wawili yeye na shemeji yake na kushambuliwa na visu hadi kusababisha umauti.
Mabula aliyetamba na kikosi cha Mtibwa kilichofanikiwa kuwa mabingwa wa bara mara mbili mfululizo 1999 na 2000 anatarajia kuzikwa Jumatatu jijini Dar es Salaam, kwa niaba ya mtandao huu unatoa pole kwa wafiwa na kulaani vikali vitendo vya mauaji ya kinyama