CHIRWA AIGAWA YANGA
Na Salum Fikiri Jr, DAR ES SALAAM
MSHAMBULIAJI mpya wa mabingwa wa soka nchini Yanga SC Obrey Chirwa ameigawa timu hiyo hasa baada ya kucheza dakika 45 za mchezo wa kombe la Shirikisho barani Afrika dhidi ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Chirwa amecheza mchezo huo lakini ameshindwa kuwashawishi Wanayanga wote na kila mmoja anasema lake, mshambuliaji huyo raia wa Zambia aliyetua Yanga kwa mkataba wa miaka miwili akitokea FC Platinum ya Zimbabwe alishindwa kuifungia Yanga bao wakati ilipolala 1-0 Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.
Katibu wa Baraza la wazee la Yanga Ibrahim Akilimali alimponda nyota huyo kwa kushindwa kuonyesha cheche ikiwa amesajiliwa kwa pesa nyingi, lakini baadhi ya wanachama wa Yanga wakamshutumu mzee huyo wakidai mchezaji huyo bado anayo nafasi ya kung' ara