TELELA NJIA NYEUPE SIMBA
Na Salum Fikiri Jr, DAR ES SALAAM
YANGA imeachana na mpango wa kumuongezea mkataba kiungo wake Salum Abdul Telela "Abo Master" na sasa njia nyeupe kwa mahasimu zao Simba SC kunasa saini yake.
Telela ambaye ameonyesha kiwango kikubwa kwenye kikosi hicho cha Yanga na kuisaidia kutwaa ubingwa wa Ngao ya Jamii mara mbili mfululizo, Ligi kuu bara mara mbili mfululizo na kombe la FA, pia ameisaidia Yanga kutinga hatua ya makundi kombe la Shirikisho barani Afrika.
Mchezaji huyo mwenye nidhamu ya hali ya juu anatajwa kutemwa na kocha Hans Van der Pluijm ambaye hakuwa na maelewano naye mazuri, Simba walisikika wakimtaja kwenye usajili wao na sasa mambo yanaweza kuwa supa kwani Yanga wameshasitisha mpango wa kumpa mkataba mpya