MICHANO: USTAADH JUMA NA MUSOMA, AMEISHIA KUJENGA NYUMBA KWA MATOFALI YA MABARAFU
Na Mkola Man, TANGA
YAP.....yap....yap....Michano yangu ya leo inamchana Ustaadh Juma na Musoma aliyekuwa meneja wa kundi la muziki lijulikanalo kwa jina la Watanashati Family akiwamo PNC, Kitale, Dogo Janja na wengine.
Hakika meneja huyu hakuwa nania ama malengo ya kweli kwa wasanii wake, alichokifanya ni kujenga nyumba kwa kutumia matofali ya mabarafu, akijuwa wazi jua likiwaka yatayeyuka.
Hakuweka bajeti ya kutosha yenye lengo la mafanikio, kiukweli alikuwa anatafuta jina tu, mameneja kama hawa wapo wengi wameshindwa kupata mafanikio kwa mfumo wa mameneja feki kama wa Ustaadh Juma.
Ila mwisho wa siku lawama uwakumba wasanii Michano inawachana mameneja wote feki, Tukutane wiki ijayo ni mimi Mkola Man........MwanaTanga