YANGA WAJIFUA KINOMA ANTALYA
Na Ikram Khamees, ANTALYA
MABINGWA wa soka Tanzania bara wanaendelea kujifua mjini hapa kujiandaa na mchezo wao wa kwanza kombe la Shirikisho barani Afrika dhidi ya MO Bejaia ya Algeria.
Yanga imeweka kambi yake katika jiji la Antalya ikifikia kwenye hoteli ya kifahali ya Rui, kocha mkuu wa mabingwa hao Mholanzi Hans Van der Pluijm amesema kambi yao ya Uturuki itawapa ushindi dhidi ya Waargeria hao.
Kikosi hicho kinafanya mazoezi makali kuanzia asubuhi, jioni mpaka usiku na wachezaji wote wanaonekana kuwa ari, kasi na nguvu kuhakikisha wanatekeleza maagizo ya mwalimu wao Hans na msaidizi wake Juma Mwambusi