Machapisho

Masaka, Clara Luvanga kurejea bongo

Picha
Hii leo kimetangazwa kikosi cha timu ya taifa ya wanawake ya Tanzania, Twiga Stars kitakachoingia kambini kuanzia Oktoba 1, 2026, kwa ajili ya maandalizi ya michezo miwili ya kufuzu kwa Mashindano ya Olimpiki dhidi ya Botswana. Tanzania itacheza mchezo wa kwanza ugenini Oktoba 9 na kurejea nyumbani kwa mchezo wa pili Oktoba 13. Miongoni mwa majina yaliyopewa nafasi kwenye kikosi hicho ni Aisha Masaka, ambaye amerejea baada ya kukosekana kwa muda mrefu takribani miaka miwili kutokana na majeraha yake ya muda mrefu, pamoja na Clara Luvanga, ambaye pia amerejea kwenye kikosi cha Taifa baada ya kutokuwapo katika baadhi ya machaguo yaliyopita. Katika kikosi hicho, uwakilishi wa klabu ; JKT Queens — wachezaji 7 Simba Queens — wachezaji 6 Fountain Gate Princess — mchezaji 1 Yanga Princess — mchezaji 1 Mashujaa Queens,Tausi FC,Ceasia Queens,Bunda Queens,Alliance Girls hakuna mchezaji aliejumuishwa. Baadhi ya wachezaji waliokosekana baada ya kuwa sehemu ya kikosi cha Twiga Stars kwa muda mrefu ...

ILI KULETA HAMASA KUIONA STARS, MASHABIKI WANGEINGIA BURE

Picha
Na Prince Hoza Matua HAMASA ni kitu muhimu sana katika kuhakikisha jambo lako linaenda vizuri, timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars imepoteza mvuto wake ambao umefanya mashabiki kutokwenda viwanjani kuona mechi zao. Ni kweli sasa hivi kuna wimbi la mashabiki kutokwenda viwanjani iwe inacheza timu ya taifa, hata mechi nyingine za ligi au kirafiki, lakini pia mashabiki siku hizi hawaudhurii hata mechi za Simba ama Yanga. Mechi ambayo haikauki watu ni Simba na Yanga, lakini timu ya taifa, imepoteza kabisa mvuto wake, siyo Tanzania pekee iliyopoteza mvuto hata mataifa mengine vile vile nayo hawapati maudhurio viwanjani. Nikija kwa upande wa Tanzania, nchi niliyozaliwa ambapo wananchi wake wanapenda mpira, miaka ya karibuni mashabiki wa Tanzania wanajaa kwa wingi viwanjani kiasi kwamba Shirikisho la soka Afrika, CAF na FIFA zinaichagua Tanzania kuwa nchi yenye mashabiki wa soka. Ila Cha kushangaza siku za karibuni idadi ya mashabiki nchini imezidi kupungua viwanjani, na timu ya taifa, Tai...

M'mombwa, Mnoga waungana na wenzao Stars

Picha
Charles M’mombwa, Miano Danilo pamoja na Haji Mnoga leo wameungana na wenzao kwenye kambi ya Taifa Stars kuendelea na maandalizi ya michezo ijayo. Taifa Stars inajiandaa kucheza michezo miwili ya kufuzu AFCON 2027, sambamba na michezo miwili ya kirafiki ambayo inatarajiwa kuchezwa nchini Morocco mwanzoni mwa mwezi

Bernard Kamungo aiwahi Guinea Bissau

Picha
Kinda wa Tanzania ambaye anacheza Ligi Kuu ya Marekani kwenye Klabu ya FC Dallas Bernard Kamungo tayari amewasili nchini leo kwaajili ya mechi mbili za kufuzu Michuano ya AFCON 2027 pamoja na mchezo wa kirafiki Taifa Stars ambao ni miongoni mwa mataifa matatu ambayo yataandaa michuano hiyo mwakani licha ya kuwa na uhakika wa kushiriki itacheza mechi mbili za Kufuzu AFCON 2027 dhidi ya Guinea Bissau pamoja na Madagascar lakini pia mchezo wa kirafiki dhidi ya Ghana Ikumbukwe kuwa Bernard Kamungo mwenye umri wa miaka 24 hii ni kwa mara ya kwanza anafika kwenye kambi ya Timu ya Taifa ya Tanzania na kama atapata nafasi ya kucheza basi ataandika rekodi mpya ya kucheza kwa mara ya kwanza ndani ya Ardhi na jezi ya Taifa lake la Tanzania.

Geita Gold na matokeo ya kushangaza Ligi Kuu bara

Picha
Klabu ya Geita Gold kutoka mkoani Geita ni miongoni mwa timu iliyocheza na timu zote tatu kubwa kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu. Haya ni matokeo yao ya Jumla katika michezo Sita ya Ligi mpaka sasa ✅️1-0 vs MBEYA CITY ❌️1-0 vs NAMUNGO FC ✅️6-2 vs KAGERA SUGAR 🤝2-2 vs AZAM FC ❌️2-0 vs SIMBA SC ❌️1-0 vs YANGA SC Kwenye timu za madaraja ya kati wamechukua alama sita na wamecheza mchezo mmoja tu nyumbani huku wakiwa na alama saba katika nafasi ya tisa. Licha ya kucheza na Vigogo wote lakini idadi kubwa ya mabao waliyoruhusu Kwenye mchezo mmoja ni mawili pekee.

Hersi akumbushia kipigo cha Simba 4-1

Picha
Rais wa Yanga , Eng. Hersi Said, amesema siku moja baada ya Yanga kupoteza mchezo kwa mabao 4-1, Feisal Salum “Feitoto” alimweleza kuwa baadhi ya wachezaji walikuwa wamehusika katika “kuuza” mchezo huo. Hersi: “Baadaye nilikuja kuambiwa na Feisal kuwa kuna baadhi ya wachezaji wameuza mechi. Alinitajia majina na baada ya kufanya utafiti nikagundua kweli siku moja kabla ya mechi baadhi yao walikutana na mmoja wa viongozi wa Simba hotelini.” Hersi amesema kipigo hicho kilimuumiza sana, lakini baadaye Yanga ilipata nafasi ya kulipa kisasi kwa kuifunga Simba 5-0. “Nilijiambia ipo siku nitazilipa. Mungu mkubwa, haikuchukua miaka mingi nikalipa kwa kuwachapa goli tano.”

Chasambi ashiriki droo AFCON

Picha
Mchezaji wa Singida BS, Ladack Chasambi, alishiriki droo ya Kufuzu #AFCON kwa vijana chini ya miaka 17 kwa ukanda wa CECAFA ambayo ilifanyika leo Septemba 23, 2026 katika studio za #AzamTV. Chasambi alikuwa Mchezaji Bora (MVP) wakati shindano hilo lilipofanyika kwa mara ya kwanza mwaka 2018.