Bernard Kamungo aiwahi Guinea Bissau

Kinda wa Tanzania ambaye anacheza Ligi Kuu ya Marekani kwenye Klabu ya FC Dallas Bernard Kamungo tayari amewasili nchini leo kwaajili ya mechi mbili za kufuzu Michuano ya AFCON 2027 pamoja na mchezo wa kirafiki

Taifa Stars ambao ni miongoni mwa mataifa matatu ambayo yataandaa michuano hiyo mwakani licha ya kuwa na uhakika wa kushiriki itacheza mechi mbili za Kufuzu AFCON 2027 dhidi ya Guinea Bissau pamoja na Madagascar lakini pia mchezo wa kirafiki dhidi ya Ghana

Ikumbukwe kuwa Bernard Kamungo mwenye umri wa miaka 24 hii ni kwa mara ya kwanza anafika kwenye kambi ya Timu ya Taifa ya Tanzania na kama atapata nafasi ya kucheza basi ataandika rekodi mpya ya kucheza kwa mara ya kwanza ndani ya Ardhi na jezi ya Taifa lake la Tanzania.


Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FIFA yatoa orodha ya vilabu bora duniani, Simba na Yanga zachuana vikali

Kocha Simba anataka wachezaji wapya watano

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI