ILI KULETA HAMASA KUIONA STARS, MASHABIKI WANGEINGIA BURE

Na Prince Hoza Matua

HAMASA ni kitu muhimu sana katika kuhakikisha jambo lako linaenda vizuri, timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars imepoteza mvuto wake ambao umefanya mashabiki kutokwenda viwanjani kuona mechi zao.

Ni kweli sasa hivi kuna wimbi la mashabiki kutokwenda viwanjani iwe inacheza timu ya taifa, hata mechi nyingine za ligi au kirafiki, lakini pia mashabiki siku hizi hawaudhurii hata mechi za Simba ama Yanga.

Mechi ambayo haikauki watu ni Simba na Yanga, lakini timu ya taifa, imepoteza kabisa mvuto wake, siyo Tanzania pekee iliyopoteza mvuto hata mataifa mengine vile vile nayo hawapati maudhurio viwanjani.

Nikija kwa upande wa Tanzania, nchi niliyozaliwa ambapo wananchi wake wanapenda mpira, miaka ya karibuni mashabiki wa Tanzania wanajaa kwa wingi viwanjani kiasi kwamba Shirikisho la soka Afrika, CAF na FIFA zinaichagua Tanzania kuwa nchi yenye mashabiki wa soka.

Ila Cha kushangaza siku za karibuni idadi ya mashabiki nchini imezidi kupungua viwanjani, na timu ya taifa, Taifa Stars inakosa watazamaji, kitendo cha kukosa watazamaji kinashangaza sana isitoshe gharama za kiingilio ziko chini.

Timu ya taifa inayonolewa na Miguel Gamondi raia wa Argentina, ambayo katika AFCON za 2025 zilizofanyika Ivory Coast, ilifika hatua ya 16 bora ikiwa ni historia kwa nchi kufanya hivyo.

Watanzania walikuwa wanaenda kwa wingi viwanjani kuiona timu ya taifa, Taifa Stars, ikicheza na ilikuwa inafungwa, lakini hawakauki viwanjani kuiona timu hiyo, lakini sasa timu inafanya vizuri tena ikicheza na mataifa makubwa kama Nigeria, Morocco na nyinginezo hamasa kwa mashabiki imepotea.

Sasa kwa kuona hivyo na nikiwa kama mwandishi nimeona nitoe ushauri kwa Shirikisho la soka nchini, TFF kufikiria kuingiza mashabiki bure, kuna ulazima wa kuingiza mashabiki bure mechi hizi za kufuzu AFCON 2027 ambazo zitafanyikia Tanzania.

Najua Tanzania ni miongoni mwa nchi mwenyeji zikiwemo Kenya na Uganda, hata ilitokea timu yetu imepoteza mechi zote mbili dhidi ya Guinea Bissau na Madagascar bado tutashiriki fainali hizo kwakuwa mwenyeji.

Mechi hizo tutakazocheza nyumbani ni vema mashabiki waingie bure Ili kurudisha hamasa.
ALAMSIKI 


Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FIFA yatoa orodha ya vilabu bora duniani, Simba na Yanga zachuana vikali

Kocha Simba anataka wachezaji wapya watano

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI