Hersi akumbushia kipigo cha Simba 4-1
Rais wa Yanga , Eng. Hersi Said, amesema siku moja baada ya Yanga kupoteza mchezo kwa mabao 4-1, Feisal Salum “Feitoto” alimweleza kuwa baadhi ya wachezaji walikuwa wamehusika katika “kuuza” mchezo huo.
Hersi: “Baadaye nilikuja kuambiwa na Feisal kuwa kuna baadhi ya wachezaji wameuza mechi. Alinitajia majina na baada ya kufanya utafiti nikagundua kweli siku moja kabla ya mechi baadhi yao walikutana na mmoja wa viongozi wa Simba hotelini.”
Hersi amesema kipigo hicho kilimuumiza sana, lakini baadaye Yanga ilipata nafasi ya kulipa kisasi kwa kuifunga Simba 5-0.
“Nilijiambia ipo siku nitazilipa. Mungu mkubwa, haikuchukua miaka mingi nikalipa kwa kuwachapa goli tano.”
