Masaka, Clara Luvanga kurejea bongo


Hii leo kimetangazwa kikosi cha timu ya taifa ya wanawake ya Tanzania, Twiga Stars kitakachoingia kambini kuanzia Oktoba 1, 2026, kwa ajili ya maandalizi ya michezo miwili ya kufuzu kwa Mashindano ya Olimpiki dhidi ya Botswana. Tanzania itacheza mchezo wa kwanza ugenini Oktoba 9 na kurejea nyumbani kwa mchezo wa pili Oktoba 13.

Miongoni mwa majina yaliyopewa nafasi kwenye kikosi hicho ni Aisha Masaka, ambaye amerejea baada ya kukosekana kwa muda mrefu takribani miaka miwili kutokana na majeraha yake ya muda mrefu, pamoja na Clara Luvanga, ambaye pia amerejea kwenye kikosi cha Taifa baada ya kutokuwapo katika baadhi ya machaguo yaliyopita.

Katika kikosi hicho, uwakilishi wa klabu ;

JKT Queens — wachezaji 7

Simba Queens — wachezaji 6

Fountain Gate Princess — mchezaji 1

Yanga Princess — mchezaji 1

Mashujaa Queens,Tausi FC,Ceasia Queens,Bunda Queens,Alliance Girls hakuna mchezaji aliejumuishwa.

Baadhi ya wachezaji waliokosekana baada ya kuwa sehemu ya kikosi cha Twiga Stars kwa muda mrefu ni

Asha Mrisho
Janeth Pangamwene
Donisia Minja
Lidya Kabambo
Jamila Rajab
Stumai Abdallah

Kurejea kwa Masaka na Luvanga kunaongeza pia sura mpya katika kikosi kinachoanza maandalizi ya safari ya Tanzania katika kampeni ya kufuzu Olimpiki.



Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FIFA yatoa orodha ya vilabu bora duniani, Simba na Yanga zachuana vikali

Kocha Simba anataka wachezaji wapya watano

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI