Machapisho

Kocha DR Congo aja kumrithi Pantev, Simba

Picha
Taarifa za kiutondoti bado zinaeleza kuwa Mnyama Simba SC bado yupo kwenye rada za kumnasa kocha Sebastien Serge Louis kuwa kocha mkuu, Louis anakuja kurithi mikoba ya Meneja Dimitar Pantev ambaye yupo kwenye kikosi cha Mnyama, Louis atakuwa kocha mkuu huku akisaidiana na Seleman Matola kwenye benchi hilo, Kwasasa Louis anakinoa kikosi cha timu ya taifa ya DR Congo.

Coastal Union yailalua Mbeya City

Picha
TIMU ya Coastal Union imeibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Mbeya City katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara mchana wa leo Uwanja wa Mkwakwani Jijini Tanga. Mabao yote ya Coastal Union yamefungwa na mshambuliaji Maabad Maulid Maabad dakika ya tatu na 42 na kwa ushindi huo wanatimiza pointi nane katika mchezo wa sita na kusogea nafasi ya saba wakiizidi tu wastani wa mabao Mbeya City ambao wamecheza mechi nane. Mara baada ya mchezi huo, Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) lilitoa taarifa ya kuufungia Uwanja wa Mkwakwani kutokana na ubovu wa eneo la kuchezea (Pitch).

Fountain Gate yaididimiza Tanzania Prisons

Picha
TIMU ya Fountain Gate imeibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya Tanzania Prisons katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara jioni ya leo Uwanka wa Tanzanite Kwaraa, Babati mkoani Manyara . Pongezi kwa mfungaji wa bao hilo pekee, mshambuliaji Mnigeria, Obasi Macdonald Chukwunonye dakika ya 43 na kwa ushindi huo Fountain Gate wanafikisha pointi 10 katika mchezo wa nane na kusogea nafasi ya tano. Kwa upande wao Tanzania Prisons baada ya kupoteza mchezo huo wanabaki na pointi zao sita kufuatia kucheza mechi sita pia na kushuka kwa nafasi moja hadi ya 12.

CCM Mkwakwani yafungiwa tena

Picha
SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limeufungia Uwanja wa Mkwakwani Jijini Tanga kwa matumizi ya mechi za Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara kutokana na ubovu wa eneo la kuchezea (Pitch). Taarifa ya TFF kuufungia Uwanja ilitolewa muda mfupi tu baada ya mchezo wa Ligi Kuu — wenyeji, Coastal Union wakiibuka na ushindi wa 2-0 dhidi ya Mbeya City kwenye Uwanja huo.

Siri zavuja, mkakati wa kumng' oa MO, Simba waiva

Picha
Zachini kabisa naambiwa baadhi ya viongozi wa Simba wanaendelea na vikao kimya kimya Ili kumuondoa Mohamed Dewji maarufu MO ndani ya klabu hiyo kama mwekezaji. Inasemekaka kuwa Mo ndo amekuwa sababu ya klabu hiyo kuzidi kushuka kiwango msimu Kwa msimu kutokana na uwekezaji wake ndani ya klabu kuwa mdogo. Hata suala la CEO wa Simba, zubeda Sakuru kuongezewa mkataba Unaambiwa MO haja husika na chochote na wala hana taarifa. Awamu hii viongozi wako serious kumuondoa MO na wamesema hawatarudi nyuma ni bora klabu itembeze bakuli.

Ndimbo aula CAF

Picha
Ofisa Habari na Mawasiliano TFF, Cliford Mario Ndimbo ameteuliwa na CAF kuwa Ofisa Habari wa mchezo wa Makundi Kombe la Shirikisho Afrika (CAFCC) Singida BS (Tanzania) vs Stellenbosch (Afrika Kusini) utakaochezwa uwanja wa Amaan, Zanzibar, Novemba 30,2025

Guinea yakwaa kisiki CAS

Picha
Miezi michache iliyopita Guinea ilikata rufaa ikitaka Tanzania itupwe nje kwa madai ya kuvunja kanuni katika mchezo wa mwisho wa kufuzu AFCON uliozikutanisha timu hizo wakitumaini kuchukua nafasi ya Tanzania katika michuano ya AFCON ambayo itatimua vumbi disemba 2025 nchini Morocco. Lakini Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo (CAS) imeitupilia mbali rufaa hiyo, ikimaanisha Tanzania inabaki imefuzu na itacheza michuano hiyo kama ilivyopangwa. Tanzania imepangwa kundi C na timu za Tunisia,Nigeria na Uganda.