Miezi michache iliyopita Guinea ilikata rufaa ikitaka Tanzania itupwe nje kwa madai ya kuvunja kanuni katika mchezo wa mwisho wa kufuzu AFCON uliozikutanisha timu hizo wakitumaini kuchukua nafasi ya Tanzania katika michuano ya AFCON ambayo itatimua vumbi disemba 2025 nchini Morocco.
Lakini Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo (CAS) imeitupilia mbali rufaa hiyo, ikimaanisha Tanzania inabaki imefuzu na itacheza michuano hiyo kama ilivyopangwa.
Tanzania imepangwa kundi C na timu za Tunisia,Nigeria na Uganda.
