TIMU ya Coastal Union imeibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Mbeya City katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara mchana wa leo Uwanja wa Mkwakwani Jijini Tanga.
Mabao yote ya Coastal Union yamefungwa na mshambuliaji Maabad Maulid Maabad dakika ya tatu na 42 na kwa ushindi huo wanatimiza pointi nane katika mchezo wa sita na kusogea nafasi ya saba wakiizidi tu wastani wa mabao Mbeya City ambao wamecheza mechi nane.
Mara baada ya mchezi huo, Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) lilitoa taarifa ya kuufungia Uwanja wa Mkwakwani kutokana na ubovu wa eneo la kuchezea (Pitch).
