SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limeufungia Uwanja wa Mkwakwani Jijini Tanga kwa matumizi ya mechi za Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara kutokana na ubovu wa eneo la kuchezea (Pitch).
Taarifa ya TFF kuufungia Uwanja ilitolewa muda mfupi tu baada ya mchezo wa Ligi Kuu — wenyeji, Coastal Union wakiibuka na ushindi wa 2-0 dhidi ya Mbeya City kwenye Uwanja huo.
