TIMU ya Fountain Gate imeibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya Tanzania Prisons katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara jioni ya leo Uwanka wa Tanzanite Kwaraa, Babati mkoani Manyara
.
Pongezi kwa mfungaji wa bao hilo pekee, mshambuliaji Mnigeria, Obasi Macdonald Chukwunonye dakika ya 43 na kwa ushindi huo Fountain Gate wanafikisha pointi 10 katika mchezo wa nane na kusogea nafasi ya tano.
Kwa upande wao Tanzania Prisons baada ya kupoteza mchezo huo wanabaki na pointi zao sita kufuatia kucheza mechi sita pia na kushuka kwa nafasi moja hadi ya 12.
