Machapisho

SIMBA NA ASANTE KOTOKO HAPATOSHI TAIFA

Picha
Na Mwandishi Wetu. Dar es Salaam Mabingwa wa soka nchini Simba SC wanatelemka uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam jioni ya leo kuumana na Asante Kotoko ya Ghana mchezo wa kirafiki kuadhimisha Simba Day. Asante Kotoko iliwasili jana tayari kwa mchezo huo, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa ndiye mgeni wa heshima, kuelekea katika tamasha hilo kikosi cha Simba kiliwasili nchini Jumapili kikitokea Uturuki ambapo kiliweka kambi wiki mbili. Kocha mkuu wa Simba Mbelgiji Patrick J Aussems jana aliwaambia waandishi wa habari kuwa atautumia mchezo huo kupata taswira ya kikosi chake, mchezo huo utaanza saa 10:00 na lengo ni kutambulisha wachezaji wapya na jezi mpya

MOROCCO AIGOMEA SINGIDA UNITED

Picha
Na Saida Salum. Dar es Salaam Kocha mkuu wa klabu ya soka ya Singida United  Hemed Suleiman Morocco ameamua kuigomea klabu yake baada ya kushindwa kumtimizia mahitaji yake kama walivyokubaliana hapo mwanzo. Akizungumza kwa njia ya simu kutoka kwao Zanzibar, Morocco amesema ameamua kugoma kuiongoza timu hiyo kwa sababu hajalipwa stahiki zake hivyo ameshindwa kuambatana na kikosi jijini Mwanza ambapo kimeweka kambi. Morocco ambaye ni kocha wa timu ya taifa ya Zanzibar, Zanzibar Heroes amedai hawezi kuripoti kambini mpaka pale atakapolipwa stahiki zake kwani ameanza kuingia shaka na viongozi wa timu hiyo kwa kuchelewa kumkamilishia mahitaji yake

Ali Kiba aahidi makubwa Coastal Union

Picha
Na Mkola Man. Tanga Mchezaji mpya wa Coastal Union ya Tanga Ali Saleh Kiba maarufu King Kiba ameahidi kuifanyia mambo makubwa klabu yake ya Coastal Union kwakuwa ndiy pekee iliyoweza kumpa heshima kubwa na kumsajili. Akizungumza na Mtandao hu, Kiba amesema Coastal Union imempa heshima kubwa kwa kumsajili kwa Mara ya kwanza kuchezaLigi Kuu kwani soka alilokuwa akicheza ni lmchangani tu. Kiba amesema kwa kiwango alichonacho atawashangaza Watanzania na kukubali mileanachokifanya, Kiba ni mwanamuziki wa miondoko ya bongofleva na amekuwa akifanya vizuri mno tungo sake

KCB kudhamini Ligi Kuu Bara

Picha
Na Prince Hoza. Dar es Salaam Benki ya biashara ya Kenya (KCB) imeingia mkataba na Shirikisho la mpira wa miguu nchini (TFF) wa kuidhamini Ligi Kuu Tanzania Bara wenye thamani ya shilingi Milioni 409 za Kitanzania. Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya utiaji saini ya mkataba huo, Rais wa Shirikisho la soka nchini Wallace Karia amesema KCB imeingia mkataba wa kuidhamini Ligi Kuu Bara 2018/2019 ikiwa kama mdhamini mwenza huku jitihada zikiendelea kumpata mdhamini mkuu wa ligi hiyo. Mkataba huo ulisainiwa asubuhi katika hoteli ya Serena iliyopo mjini Dar es Salaam, kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom bado haijathibitisha kama itadhamini tena ligi hiyo ama itaachana moja kwa moja na udhamini huo hasa baada ya mkataba wao kumalizika

Baada ya kipigo toka kwa Gormahia, kocha Yanga aishushia lawama TFF

Picha
Na Ikram Khamees. Dar es Salaam Kocha msaidizi wa klabu ya soka ya Yanga SC, Mzambia Noel Mwandila amelishushia lawama Shirikisho la soka nchini TFF kwa kitendo cha kuwachukua wachezaji wao jana na kukaa nao kwa zaidi ya masaa 10 wakati wakifahamu walikuwa na mchezo mgumu dhidi ya Gor Mahia siku inayofuata. Kwa mujibu wa Mwandila, TFF iliwatoa kwenye kambi ya Yanga nyota sita wa timu ya taifa kwa ajili ya kwenda kupiga picha saa 8 mchana ambapo amesema walirejea kambini saa 7 usiku. Mwandila alikuwa akielezea umuhimu wa TFF kutoa ushirikiano kwa timu hasa zinapoliwakilisha taifa huku akisema kuwa tukio hilo linaweza kuwa limewaathiri kwavile wachezaji hawakupata muda wa kupumzika. Yanga imepoteza mchezo huo kwa kufungwa mabao 3-2.

KISPOTI

Picha
Mnashangaa ya Mwigulu na Yanga mnasahau ya Bakhresa kwa Simba Na Prince Hoza HIVI karibuni mbunge wa Iramba Mashariki kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) Dr Mwigulu Lameck Nchemba ambaye pia in kiongozi mkuu wa klabu ya soka yaSingida United inayoshiriki Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bars aliamua kuwatunuku Yanga SC wachezaji watatu ambapo yeye mwenyewe alisema in msaada wake kwa klabu hiyo. Dr Mwigulu alianza kuwapa Yanga kiungo aliyesajiliwa na klabu take ya Singida United, Fesal Salum Abdallah "Fei Toto" katika maelezo yake Dr Mwigulu alisema aliamua kuhamisha leseni ya Fei Toto Singida United na kuipeleka kwa Yanga SC. Singida United ilimsajili Fei Toto kwa kandarasi ya miaka mitatu akitokea JKU ya Zanzibar lakini Sikh so nyingi Yanga nao wakatangaza kumsajili, Dr Mwigulu ameweka wazi kuwa gharama zote walizomlipa Fei Toto zitatumiwa na Yanga na wala hawatamdai. Pia Dr Mwigulu ambaye amewahi kuwa waziri wa mambo ya ndani ya nchi kabla ya Raid wa Jamhuri ya muungano wa ...

GORMAHIA YAINYUKA TENA YANGA

Picha
Na Ikram Khamees. Dar es Salaam Klabu bingwa ya soka nchini Kenya ya Gormahia usiku huu imeinyuka bila huruma Yanga SC ya Tanzania mabao 3-2 mchezo wa kombe la Shirikisho barani Afrika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Gormahia ilitangulia kujipatia bao la kwanza lililofungwa kunako sekunde ya 23 kipindi cha kwanza na mshambuliaji George Odhiambo ambaye alifunga lingine katika dakika ya 40 na timu hizo zilienda kupumzika kwa matokeo hayo. Yanga walirejea na kasi mpya na kujipatia bao dakika ya 53 lililofungwa na Deus Kaseke likiwa pia ni goli la kwanza katika michuano hiyo ya pill kwa ukubwa Afrika, Jacques Tuyisenge aliifungia Gormahia goli la tatu na la ushindi dakika ya 64 kabla ya Raphael Saudi Lothi hajafunga bao la pill la Yanga dakika ya 80. Yanga leo watamlaumu kipa wao Youthe Rostand ambaye aliwaggharimu karibu magoli mawili na baadaye kocha wa Yanga akamtoa na kumwingiza Benno Kakolanya