MOROCCO AIGOMEA SINGIDA UNITED
Na Saida Salum. Dar es Salaam
Kocha mkuu wa klabu ya soka ya Singida United Hemed Suleiman Morocco ameamua kuigomea klabu yake baada ya kushindwa kumtimizia mahitaji yake kama walivyokubaliana hapo mwanzo.
Akizungumza kwa njia ya simu kutoka kwao Zanzibar, Morocco amesema ameamua kugoma kuiongoza timu hiyo kwa sababu hajalipwa stahiki zake hivyo ameshindwa kuambatana na kikosi jijini Mwanza ambapo kimeweka kambi.
Morocco ambaye ni kocha wa timu ya taifa ya Zanzibar, Zanzibar Heroes amedai hawezi kuripoti kambini mpaka pale atakapolipwa stahiki zake kwani ameanza kuingia shaka na viongozi wa timu hiyo kwa kuchelewa kumkamilishia mahitaji yake