Jayrutty yabisha hodi Rayon Sports

Kampuni ya Kitanzania Jayrutty Investment East Africa Ltd inaendelea kupanua ushawishi wake katika sekta ya michezo barani Afrika kupitia ushirikiano na klabu mbalimbali. Kwa upande wa Rayon Sports ya Rwanda,

Jayrutty imeingia makubaliano ya miaka mitano ya kuwa mshirika rasmi katika usambazaji wa jezi na vifaa vya klabu hiyo, katika mkataba unaoripotiwa kuwa na thamani ya Dola milioni 3.5.

Rayon Sports pia imeonekana ikitumia jezi mpya za Jayrutty wakati wa safari ya kuelekea Cameroon, huku kampuni hiyo ikishirikiana na Umbro katika utengenezaji wa jezi hizo. Jayrutty pia ina uhusiano wa kibiashara na Simba SC, ikiwa miongoni mwa kampuni zinazojihusisha na mavazi pamoja na bidhaa za michezo.

Hatua hizi zinaendelea kuifanya Jayrutty kuwa miongoni mwa kampuni za Kitanzania zinazojenga ushawishi katika sekta ya michezo nje ya mipaka ya Tanzania. Kutoka Tanzania hadi Rwanda na katika soka la kimataifa Jayrutty inaendelea kujenga jina barani Afrika.


Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FIFA yatoa orodha ya vilabu bora duniani, Simba na Yanga zachuana vikali

Kocha Simba anataka wachezaji wapya watano

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI