Pitso Mosimane awa kocha mkuu Bafana Bafana
Shirikisho la Soka la Afrika Kusini (SAFA) limemtambulisha rasmi mkufunzi Pitso Mosimane kuwa kocha mkuu mpya wa Timu ya Taifa ya Afrika Kusini, (Bafana Bafana) akichukua mikoba ya Hugo Broos aliyeondoka baada ya mkataba wake kutamatika.
Rais wa SAFA, Danny Jordaan, amemtangaza rasmi Mosimane leo Septemba 1, 2026 ikiwa ni urejeo wa pili kwa kocha huyo wa zamani wa Mamelodi Sundowns na Al Ahly kuinoa Bafana Bafana tangu alipokiongoza kikosi hicho kuanzia 2010 hadi 2012.
