Machapisho

Ismail Mgunda bado sana kiwango+ Barker

Picha
Kocha mkuu wa klabu ya Simba SC, Steve Barker, amesema mchezaji kama Ismaïl Mgumda anahitaji uangalizi mkubwa, kwani bado kuna baadhi ya vitu vinapotea kwake akiwa uwanjani. Amesema mara nyingi humpa nafasi ili asije akawa mchezaji wa kukaa benchi, huku akiamini kuwa akipata nafasi zaidi ataweza kuonyesha uwezo wake vizuri. “Siwezi kumchoka mchezaji wangu. Mbinu zangu ameanza kuzifanya vizuri na tukiwa kambini tutafanya namna yoyote kumpa nafasi ya kucheza ili kupata umakini zaidi uwanjani. “Mechi za kirafiki zinaweza kumpa ujasiri kuwa ni mchezaji anayehitajika katika kikosi cha kwanza dhidi ya Yanga SC. Nitampa nafasi kubwa ya kucheza, si kwa mchezo huo pekee. “Nina wachezaji watatu ambao watakuwa mbele ya mfumo wangu; Maema, Mgumda pamoja na Doumbia. Hawa ni wachezaji ambao ukiwapa mbinu wanafanya kweli. “Jua kuwa mchezaji unapomwacha benchi, kiwango kinazidi kushuka, lakini ukimpa nafasi anaona kumbe naweza kufanya kitu. Kwa hiyo tusubiri kuona mazuri ndani ya kikosi chetu.” — Stev...

Yanga SC wafanya semina ya usalama wa watoto

Picha
Leo tumefanya semina kwa vijana ikihusisha mada mbalimbali muhimu, ikiwemo usalama na ulinzi wa watoto (Safeguarding & Child Protection), uzoefu wa safari za kimataifa pamoja na maarifa na misingi ya ufundishaji wa soka kwa vijana. Kupitia makubaliano yetu na Dulla Sports Centre ya Zanzibar katika kukuza na kuendeleza vipaji vya vijana, moja ya maeneo muhimu tuliyokubaliana ni kubadilishana uzoefu, maarifa na utaalamu kwa lengo la kuwajengea vijana mazingira bora ya kukuza vipaji vyao ndani na nje ya uwanja. Tunaamini uwekezaji katika maarifa, malezi na maendeleo ya vijana ni sehemu muhimu ya kujenga kizazi cha wachezaji wenye uwezo, nidhamu na uelewa mpana wa soka.

Watanzania wapuuze uzushi, Stars wamegomea kusafiri Morocco

Picha
Afisa Habari na Mawasiliano wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Clifford Mario Ndimbo, amewataka Watanzania kupuuza taarifa za mtandaoni zilizokuwa zikidai kuwa wachezaji wa Timu ya Taifa (Taifa Stars) wamegoma kusafiri kuelekea Morocco wakishinikiza kulipwa posho zao. Akizungumzia uvumi huo wa mgomo, Ndimbo alikanusha vikali na kusema: "Nisingependa kuzungumzia mambo ya mtandaoni. Timu hivi sasa inakabiliwa na mchezo muhimu kabisa wa pili dhidi ya Madagascar, mchezo wa kufuzu, ni mchezo mkubwa sana. Kwa hiyo, tunachokiangalia ni kwamba timu ya taifa ikishakwenda inapata matokeo mazuri." Akihojiwa kupitia Global TV wakati kikosi kikiondoka, Ndimbo alithibitisha kuwa mipango yote ya safari imeenda vizuri na timu ipo tayari kwa mapambano hayo ya ugenini ili kusaka pointi tatu muhimu.

Waandaaji miaka 30 ya bongofleva wamlipia faini Dudubaya

Picha
Waandaaji wa Tamasha la Miaka 30 ya BongoFleva wametangaza kutekeleza adhabu iliyotolewa na Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) kwa kumlipia kiasi cha shilingi milioni tatu Msanii Godfrey Tumaini maarufu kama Dudu Baya. Kupitia taarifa iliyotolewa leo na Mmoja wa Waratibu wa Tamasha hilo, Madee Ali amesema baada ya kupokea maamuzi ya BASATA, wamekubali kuyatekeleza na kwa haraka kulipa faini iliyotolewa kwao, pamoja na kulipa faini iliyotolewa kwa Msanii Dudu Baya. Waandaaji hao wameihakikishia BASATA pamoja na Wadau wa sanaa Nchini kuwa wanaheshimu maamuzi yaliyotolewa na wataendelea kutekeleza wajibu wao kwa kuzingatia taratibu na Sheria zilizowekwa. Aidha, wameeleza kuwa ushirikiano, uwajibikaji na uzingatiaji wa Sheria ni miongoni mwa misingi muhimu katika kulinda, kukuza na kuendeleza sekta ya sanaa Nchini. “Tunatoa shukrani kwa BASATA na Wadau wote kwa ushirikiano wao, huku tukiahidi kuendelea kushirikiana na mamlaka husika katika kuhakikisha Sekta ya Sanaa inakua na kuendelezwa kw...

Simba Marathon waanza kupatiwa vifaa

Picha
Washiriki wa 𝐒imba Marathon 2026 tayari wameanza kuchukua vifaa vyao vya kushiriki mbio hizi kubwa. Zoezi la ugawaji litaendelea kesho Jumapili ndani ya Mlimani City kuanzia saa 3:30 asubuhi hadi saa 2:00 usiku we

Mwamnyeto ashindwa kusafiri ghafla

Picha
Wakati timu ya Taifa ikiondoka Uwanja wa Ndege wa JK Nyerere (DSM) Kuelekea Morocco kwaajili ya kufuzu Afcon dhidi ya Madagascar, Mlinzi na nahodha wa kikosi hicho Bakari Nondo Mwamnyeto amepata dharura muda mfupi kabla ya kuanza kuandoka kuelekea Morocco dharura ambayo imesababisha asisafiri na wachezaji wenzake kuelekea Morocco.

Alikamwe amchangia Dudubaya

Picha
Msemaji wa klabu ya Yanga, Ali Kamwe amchangia msanii Dudu Baya Tsh 10,000 ikiwa ni kampeni ya kumsaidia kulipa deni la milioni tatu ikiwa ni kama Faini kutoka BASATA. Inawezekana Alikamwe ameguswa na Dudubaya kwani mwanahatakati mwingine aitwaye Zungu naye ameguswa na Dudubaya na anawataka Watanzania kumchangia.