Ismail Mgunda bado sana kiwango+ Barker

Kocha mkuu wa klabu ya Simba SC, Steve Barker, amesema mchezaji kama Ismaïl Mgumda anahitaji uangalizi mkubwa, kwani bado kuna baadhi ya vitu vinapotea kwake akiwa uwanjani.

Amesema mara nyingi humpa nafasi ili asije akawa mchezaji wa kukaa benchi, huku akiamini kuwa akipata nafasi zaidi ataweza kuonyesha uwezo wake vizuri.

“Siwezi kumchoka mchezaji wangu. Mbinu zangu ameanza kuzifanya vizuri na tukiwa kambini tutafanya namna yoyote kumpa nafasi ya kucheza ili kupata umakini zaidi uwanjani.

“Mechi za kirafiki zinaweza kumpa ujasiri kuwa ni mchezaji anayehitajika katika kikosi cha kwanza dhidi ya Yanga SC. Nitampa nafasi kubwa ya kucheza, si kwa mchezo huo pekee.

“Nina wachezaji watatu ambao watakuwa mbele ya mfumo wangu; Maema, Mgumda pamoja na Doumbia. Hawa ni wachezaji ambao ukiwapa mbinu wanafanya kweli.

“Jua kuwa mchezaji unapomwacha benchi, kiwango kinazidi kushuka, lakini ukimpa nafasi anaona kumbe naweza kufanya kitu. Kwa hiyo tusubiri kuona mazuri ndani ya kikosi chetu.” — Steve Barker


Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FIFA yatoa orodha ya vilabu bora duniani, Simba na Yanga zachuana vikali

Kocha Simba anataka wachezaji wapya watano

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI