Watanzania wapuuze uzushi, Stars wamegomea kusafiri Morocco

Afisa Habari na Mawasiliano wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Clifford Mario Ndimbo, amewataka Watanzania kupuuza taarifa za mtandaoni zilizokuwa zikidai kuwa wachezaji wa Timu ya Taifa (Taifa Stars) wamegoma kusafiri kuelekea Morocco wakishinikiza kulipwa posho zao.

Akizungumzia uvumi huo wa mgomo, Ndimbo alikanusha vikali na kusema: "Nisingependa kuzungumzia mambo ya mtandaoni. Timu hivi sasa inakabiliwa na mchezo muhimu kabisa wa pili dhidi ya Madagascar, mchezo wa kufuzu, ni mchezo mkubwa sana. Kwa hiyo, tunachokiangalia ni kwamba timu ya taifa ikishakwenda inapata matokeo mazuri."

Akihojiwa kupitia Global TV wakati kikosi kikiondoka, Ndimbo alithibitisha kuwa mipango yote ya safari imeenda vizuri na timu ipo tayari kwa mapambano hayo ya ugenini ili kusaka pointi tatu muhimu.


Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FIFA yatoa orodha ya vilabu bora duniani, Simba na Yanga zachuana vikali

Kocha Simba anataka wachezaji wapya watano

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI