Machapisho

Aziz Ki arejea rasmi Yanga SC

Picha
Young Africans SC imemsajili kiungo Stephane Aziz Ki kutoka Al Ittihad SC kuelekea msimu ujao. Young Africans SC wanamalizia vitu kadhaa kwenye papers na masharti ya Al Ittihad SC ili waweze kumtangaza rasmi. KI Aziz hataki kuitumikia tena na tayari alishawapa taarifa mapema sana Al Ittihad SC na klabu hiyo ya Libya ilikuwa tayari kumuachia na iliheshimu mahitaji ya mchezaji huyo.

Wababe wa Yanga wakiona chamoto kwa JKT Tanzania

Picha
Wababe wa Young Africans SC, Les Aigles Du Congo ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wanapokea kichapo cha kizalendo huko Meja Janerali Isamuhyo dhidi ya Maafande wa JKT Tanzania. Ni katika mchezo wa kirafiki ikiwa ni muendelezo wa maandalizi kuelekea msimu mpya wa NBC Primier League 2026/2027. Mabao ya JKT Tanzania yamefungwa na Said Mkopi na Paul Peter Kasunda.

Fei atoweka Simba SC

Picha
Kiungo Feisal Salum atawasili Arusha, Tanzania kwaajili ya kufanyiwa summalization ya jeraha lake dogo la nyama za paja akiwa na kikosi cha Azam FC na ataukosa mchezo wa kwanza wa Azam FC dhidi ya Polisi Tanzania. Feisal Salum hatojiunga na Simba SC katika dirisha hili na ataendelea kuitumikia Azam FC kwa mkataba wa mwaka mmoja uliobaki hadi June 30, 2027 ambapo atakuwa mchezaji huru (Free agent).

AS Vita yanasa kinda Singida Black Stars

Picha
Klabu ya AS Vita Club ya DR Congo imekamilisha usajili wa kinda hatari Candidat Mapendo (20) kutoka Singida Black Stars kwa mkopo wa msimu mmoja. Mapendo amepelekwa kwa mkopo baada ya kukosa nafasi kwenye mipango ya kocha wa Singida Black Stars, Papy Kimoto. Kuna madai kwamba sababu ya kutokubalika kwake inahusishwa na ukabila, ingawa madai hayo hayajathibitishwa rasmi. Msimu uliopita, Mapendo alifunga mabao 21 na kuibuka mfungaji bora wa Ligi Kuu ya DR Congo, jambo lililoifanya Singida Black Stars kutumia kiasi kikubwa cha fedha kumsajili. Kesho Alhamisi, Mapendo anatarajiwa kuanza safari kutoka Kinshasa kuelekea Burundi, kisha ataelekea Baraka, ambako atapata nafasi ya kuiaga familia yake kabla ya kurejea kazini.

Depu atambulishwa Petro de Luanda

Picha
Mshambuliaji raia wa Angola, Laurindo Aurélio maarufu Depu, ametambulishwa rasmi kuwa mchezaji mpya wa Petro de Luanda baada ya kuondoka Yanga. Depu ametambulishwa rasmi leo Jumatano Agosti 12, 2026 ambapo inadaiwa Yanga imeingiza kitita cha dola 500,000 (Sh1.3 bilioni) kwa ajili ya usajili wa mchezaji huyo. Depu alikuwa sehemu ya kikosi cha Yanga msimu uliopita kabla ya kurejea nchini Angola kujiunga na Petro de Luanda.

Hadithi ya Seleman Mwalimu kuihama Simba usiku saa 9 na kwenda Yanga

Picha
-Kwamba Simba walikubaliana na Wydad Ac Usd 120,000 sawa na Milioni 316 kwajili ya mkataba wa mkopo wa mwaka mmoja wa mchezaji Selemani Mwalimu. Simba walikuwa tayari kutoa hiyo pesa ndio maana mchezaji akaruhusiwa kurudi Tanzania na akafikia kwenye Kambi ya Simba ambako alikuwepo mpaka jana kwenye mazoezi ya Simba pale Zanzibar. Yanga walivyopata taarifa za Simba kuchelewa kufanya malipo, wakaulizia wakaweka mezani Usd 200,000 (Milioni 527) yaani Usd 80,000 zaidi ya ile pesa waliyokubaliana na Simba...Wydad wakampigia simu Mwalimu kumwambia awaambie Simba kuna timu imeweka 200,000 hivyo Simba waongeze Usd 30,000 tu iwe Usd 150,000 (Milioni 395) Selemani Mwalimu alivyowaambia viongozi wa Simba, wakamwambia wanawachekecha tu kwasababu Yanga hawana uhitaji wa mshambuliaji tena... Baadaye Viongozi wakampigia simu Mwalimu kumwambia wamemalizana na Yanga hivyo anatakiwa kurudi Dar, ndipo akaondoka na ndege ya usiku kurudi Dar na alisaini mkataba na Yanga saa 9:45 usiku. Usd 30,000 ndiyo il...

Simba timu ya kushinda mataji+ Barker

Picha
Nimependa namna kocha wa Simba Steve Barker anavyozungumza kwa kujiamini,anasema Simba ni timu ya kushinda mataji hivyo anaamini kesho watafanya hivyo pia dhidi ya Yanga. Maneno anayozungumza yana ukweli mkubwa ndani yake,hasa ukizingatia kile ambacho ameshakifanya na Simba msimu uliopita walishinda FA mbele ya Azam, timu ambayo ilitoka kuifunga Yanga,huu ni uthibitisho wa kwanza wa kocha anachokisema. Simba hawakushinda FA peke yake walishinda mechi ya fainali ya Kombe la Muungano ambalo walicheza na Yanga. Ukichukua matukio ya Simba msimu uliopita na kocha anachokisema ni wazi kuwa ana sababu za kuzungumza kwa kujiamini sio maneno matupu tayari kuna kitu alishakifanya yeye kama yeye,ukiachana na klabu.