Hadithi ya Seleman Mwalimu kuihama Simba usiku saa 9 na kwenda Yanga
-Kwamba Simba walikubaliana na Wydad Ac Usd 120,000 sawa na Milioni 316 kwajili ya mkataba wa mkopo wa mwaka mmoja wa mchezaji Selemani Mwalimu.
Simba walikuwa tayari kutoa hiyo pesa ndio maana mchezaji akaruhusiwa kurudi Tanzania na akafikia kwenye Kambi ya Simba ambako alikuwepo mpaka jana kwenye mazoezi ya Simba pale Zanzibar.
Yanga walivyopata taarifa za Simba kuchelewa kufanya malipo, wakaulizia wakaweka mezani Usd 200,000 (Milioni 527) yaani Usd 80,000 zaidi ya ile pesa waliyokubaliana na Simba...Wydad wakampigia simu Mwalimu kumwambia awaambie Simba kuna timu imeweka 200,000 hivyo Simba waongeze Usd 30,000 tu iwe Usd 150,000 (Milioni 395)
Selemani Mwalimu alivyowaambia viongozi wa Simba, wakamwambia wanawachekecha tu kwasababu Yanga hawana uhitaji wa mshambuliaji tena...
Baadaye Viongozi wakampigia simu Mwalimu kumwambia wamemalizana na Yanga hivyo anatakiwa kurudi Dar, ndipo akaondoka na ndege ya usiku kurudi Dar na alisaini mkataba na Yanga saa 9:45 usiku.
Usd 30,000 ndiyo iliyovunja biashara ya Selemani Mwalimu na Simba Sc...Na hii inatokana na mambo kadhaa ambayo ni uzembe wa viongozi, Tajiri kuchelewa kutoa fedha na ujuaji.
Mwisho tunaweza kuulizana, Je Mwalimu ana thamani hiyo ya Milioni 527 kwa mkataba wa mkopo mwaka mmoja?
Kumbuka hiyo Milioni 527 ni loan fee, hapo hujaweka signing fee Milioni 160, mshahara milioni 15 kwa mwezi pamoja na gari...!
Je, ungekuwa wewe ndiye Mo Dewji ungetoa hiyo Milioni 867 kwajili ya Selemani Mwalimu ambaye Kocha Barker alikua anaamua kumtumia Mpanzu kama False No 10 huku yeye akiwa benchi? Yaani uweke milioni 867 benchi?
Nafikiri Simba bado wanaweza kurudi sokoni kutafuta striker mwingine mwenye uwezo mkubwa tu kwa gharama ya kawaida...Pale JKT Tanzania kuna Paul Peter @kasunda51 ana uwezo mkubwa tu na hata wakimchukua @william_edgar11 anaweza kuwasaidia sana pale eneo la mwisho.
#MWISO: Yanga wanafanya kazi kwa umoja sana na wanajitoa mno ndio maana walikuwa tayari kupanda dau kwa zaidi ya milioni 200
