AS Vita yanasa kinda Singida Black Stars
Klabu ya AS Vita Club ya DR Congo imekamilisha usajili wa kinda hatari Candidat Mapendo (20) kutoka Singida Black Stars kwa mkopo wa msimu mmoja.
Mapendo amepelekwa kwa mkopo baada ya kukosa nafasi kwenye mipango ya kocha wa Singida Black Stars, Papy Kimoto. Kuna madai kwamba sababu ya kutokubalika kwake inahusishwa na ukabila, ingawa madai hayo hayajathibitishwa rasmi.
Msimu uliopita, Mapendo alifunga mabao 21 na kuibuka mfungaji bora wa Ligi Kuu ya DR Congo, jambo lililoifanya Singida Black Stars kutumia kiasi kikubwa cha fedha kumsajili.
Kesho Alhamisi, Mapendo anatarajiwa kuanza safari kutoka Kinshasa kuelekea Burundi, kisha ataelekea Baraka, ambako atapata nafasi ya kuiaga familia yake kabla ya kurejea kazini.
