Simba timu ya kushinda mataji+ Barker

Nimependa namna kocha wa Simba Steve Barker anavyozungumza kwa kujiamini,anasema Simba ni timu ya kushinda mataji hivyo anaamini kesho watafanya hivyo pia dhidi ya Yanga.

Maneno anayozungumza yana ukweli mkubwa ndani yake,hasa ukizingatia kile ambacho ameshakifanya na Simba msimu uliopita walishinda FA mbele ya Azam, timu ambayo ilitoka kuifunga Yanga,huu ni uthibitisho wa kwanza wa kocha anachokisema.

Simba hawakushinda FA peke yake walishinda mechi ya fainali ya Kombe la Muungano ambalo walicheza na Yanga.

Ukichukua matukio ya Simba msimu uliopita na kocha anachokisema ni wazi kuwa ana sababu za kuzungumza kwa kujiamini sio maneno matupu tayari kuna kitu alishakifanya yeye kama yeye,ukiachana na klabu.


Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FIFA yatoa orodha ya vilabu bora duniani, Simba na Yanga zachuana vikali

Kocha Simba anataka wachezaji wapya watano

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI