Machapisho

SIMBA YAJIAPIZA KUIBOMOA NDANDA LEO

Picha
MABINGWA wa soka wa kombe la Mapinuduzi Simba SC leo jioni inashuka kwenye uwanja wa Nangwanda sijaona mjini Mtwara kukabiliana vikali na wenyeji wao Ndanda FC 'wana kuchele' timu ambayo imeipania vilivyo Simba. Uongozi wa Simba kupitia kwa msemaji wake Humphrey Nyosia umetamba kuwa ni lazima Simba iifunge Ndanda lakini kuhusu idadi ya magoli hiyo itajulikana uwanjani, akiongea na mtandao huu leo, Nyosia amesema kikosi cha Simba kimeimarika na kinaweza kushinda katika mchezo huo kwani wapinzani wao hawana ubavu hata kidogo.

Equatorial Guinea walenga Kombe la Dunia

Picha
Esteban Becker Kocha mwenye ndoto kubwa wa wenyeji wa Kombe la Mataifa ya Afrika, Equatorial Guinea, Esteban Becker amehimiza vijana wake watumie dimba hilo kama ngazi ya kufuzu Kombe la Dunia. Becker wa kutoka Argentina ambaye alichukua utawala wa Nzalang Nacional mapema mwezi huu, amekuwa na majuma mawili pekee kuandaa kikosi chake kujitosa uwanjani nyumbani wakati shindano hilo litakapongoa nanga Jumamosi dhidi ya Congo Brazzaville jijini Bata kwenye Kundi A. Ingawa kufuzu robo fainali ya awamu ya 2012 wakati nchi hiyo iliandaa kwa pamoja na Gabon ni lengo mufti, Becker anatizama mbele zaidi na azima yake ya kuwaongoza kuingia Kombe la Dunia kwa mara ya kwanza kwenye historia yao. “Naota kila wakati kushiriki Kombe la Dunia kwa hivyo bidii zangu zote zitaelekezwa kutayarisha kikosi chetu changa kuwa na nafasi ya kuwania tiketi ya kucheza dimba hilo lijalo la 2018,” Becker ambaye aliongoza...

AFCON kuanza leo Equatorial Guinea

Picha
Timu kutoka kote Afrika zimewasili nchini Equatorial Guinea wakati ambapo mechi za taifa bingwa barani zitarajiwa kung'oa nanga hii leo ikiwa ni miezi miwili tangu taifa hilo la afrika ya kati likubali kuandaa mechi hizo. Morocco ndiyo iliyokuwa iandae kombe hilo lakini badala yake ikaomba kuahirishwa kwake kutokana na hofu ya kusambaa kwa ugonjwa wa ebola.

LIGI KUU BARA KIVUMBI NA JASHO LEO, SIMBA, YANGA AU AZAM KUCHEKA?

Picha
BAADA ya michuano ya Kombe la Mapinduzi, sasa kazi inarejea kwenye. Ligi Kuu Bara.Michuano ya wiki ya Kombe la Mapinduzi mjini Zanzibar tayari imepata mbabe wake, Simba na kombe liko jijini Dar es Salaam. Vita ya vinara Mtibwa Sugar, Azam, Yanga na Simba ambao wote wana viporo katika michuano ya ligi kuu, kutokana na kuwepo katika ushiriki wa michuano ya Mapinduzi, lakini wikiendi hii- leo na kesho wanaendelea kumsaka mwali wa Ligi Kuu Bara ambaye anahifadhiwa na Azam FC. Kila upande una hofu, inajulikana kwa kuwa matokeo hayana uhakika. Mechi za mwisho zinaonyesha Yanga na Azam waliambulia sare, hali kadhalika Mtibwa Sugar wakati Simba walikutana na kichapo.

WAJERUMANI WASIKITISHWA NA BALLON D'OR

Picha
Manuel Neuer Wajerumani, waliotumai wangefagia tuzo za Fifa na kubeba Ballon D'Or, walieleza masikitiko yao Jumanne baada ya kipa wao aliyeshinda Kombe la Dunia Manuel Neuer kuibuka wa tatu katika matokeo ya mchezaji bora wa mwaka duniani wa mwaka 2014. Mreno Cristiano Ronaldo alishinda tuzo hiyo kwa mara ya pili mtawalia Jumatatu na mara ya tatu kwa jumla. Fowadi huyo wa Real Madrid alipata kura maradufu kumshinda mpinzani wake wa jadi aliyeshinda tuzo hiyo mara nne Lionel Messi, ambaye alimpiku pembamba kipa wa Bayern Munich Neuer aliyemaliza wa tatu. Neuer, aliyewika sana katika Kombe la Dunia nchini Brazil mwaka jana na pia alisaidia Bayern kushinda ligi na kombe nyumbani, amefungwa mabao manne pekee katika mechi 17 alizocheza ligini msimu huu.

GRANT NUSURA AMTIMUE AYEW

Picha
Dede Ayew  Avram Grant alikuwa nusura amtimue kiungo wa kati kutoka wa Ghana Andre Ayew kutoka kwa kambi ya timu hiyo nchini Uhispania. Kisa hicho, kilichofanyika wiki jana, kilipelekea bosi huyo wa Ghana wa miaka 59 kuanzisha shughuli ya kumfukuza mchezaji huyo kutoka Seville baada ya nyota huyo wa klabu ya Marseille kufika kambini akiwa amechelewa. Lakini naibu mwenyekiti wa kamati simamizi ya Black Stars, Kudjoe Fianoo, aliingilia kati na kumsihi kubadilisha uamuzi wake. “Mimi na [mwenyekiti wa kamati] George Afriyie tulilazimika kuingilia kati na kuomba radhi kwa niaba ya Andre Ayew kwa kufika kambini akiwa amechelewa kwa sababu Avram Grant alikuwa amekasirishwa sana na mchezaji huyo kufika Uhispania akwia amechelewa,” afisa huyo aliambia Happy FM mjini Accra.

PLUIJM APONDA MASTRAIKA WACHOYO YANGA

Picha
Kocha wa Yanga, Hans van der Pluijm amewajia juu washambuliaji wa timu hiyo kutokana na kukosa magoli mengi na amewataka kuacha uchoyo baina yao kwa manufaa ya timu. Licha ya kushinda kwa idadi kubwa ya mabao (4-0) katika mechi zao mbili za kwanza za Kombe la Mapinduzi, wachezaji wa Yanga walikuwa wakikosa magoli mengi ambayo yangeweza kuwafanya kupata ushindi mnono zaidi. Yanga ilitolewa katika robo fainali ya mashindano hayo maalum ya kuadhimisha Mapinduzi ya Zanzibar kwa goli 1-0 la dakika za lalasalama la JKU ya Zanzibar huku miamba hao wa soka wa Tanzania Bara wakiwa tayari wamekosa magoli mengi kupitia kwa washambuliaji wao Amisi Tambwe na Kpah Sherman.