AFCON kuanza leo Equatorial Guinea

Timu kutoka kote Afrika zimewasili nchini Equatorial Guinea wakati ambapo mechi za taifa bingwa barani zitarajiwa kung'oa nanga hii leo ikiwa ni miezi miwili tangu taifa hilo la afrika ya kati likubali kuandaa mechi hizo.

Morocco ndiyo iliyokuwa iandae kombe hilo lakini badala yake ikaomba kuahirishwa kwake kutokana na hofu ya kusambaa kwa ugonjwa wa ebola.


Shirikisho la kandanda barani Afrika CAF hata hivyo lilikataa ombi hilo la Morocco

Mkuu wa CAF (Hicham El Amrani) anasema kuwa kila tahadhari imechukuliwa nchini Equatorial Guinea kuwalinda watu kutokana na ugonjwa wa ebola.

Mechi ya kwanza itakuwa kati ya wenyeji Equatorial Guinea na Congo.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA