SIMBA YAJIAPIZA KUIBOMOA NDANDA LEO
MABINGWA wa soka wa kombe la Mapinuduzi Simba SC leo jioni inashuka kwenye uwanja wa Nangwanda sijaona mjini Mtwara kukabiliana vikali na wenyeji wao Ndanda FC 'wana kuchele' timu ambayo imeipania vilivyo Simba.
Uongozi wa Simba kupitia kwa msemaji wake Humphrey Nyosia umetamba kuwa ni lazima Simba iifunge Ndanda lakini kuhusu idadi ya magoli hiyo itajulikana uwanjani, akiongea na mtandao huu leo, Nyosia amesema kikosi cha Simba kimeimarika na kinaweza kushinda katika mchezo huo kwani wapinzani wao hawana ubavu hata kidogo.
Nyosia amesema Simba ni timu kubwa yenye uwezo wa kupambana na timu yoyote iwe ya ndani au nje ya nchi, 'kama tumeweza kuzifunga Mtibwa Sugar ambao ndio vinara wa ligi kuu bara sidhani kama hizi nyingine zinazoshika nafasi ya mwisho zinaweza kukuruka kwetu', alisema na kuongeza.
'Sisi ni mabingwa wa kombe la Mapinduzi kombe ambalo limeshirikisha timu zilizofanya vizuri katika ligi yake, sisi tuna kikosi kizuri kocha mzuri na tuna washangoiliaji wazuri lazima Ndanda ifungwe tu itake isitaki ushindi ni wetu, naomba baada ya mpira kwisha nipigie simu ili uone nitakavyokuthibitishia', alijitamba msemaji huyo anayejiamini zaidi.
Lakini Ndanda wao wenyewe waliamua kutoka nje kidogo ya mji huo na kudai mchezo wa leo utakuwa mgumu kwao kwani wanacheza na timu kubwa na yenye mashabiki wengi ambayo hivi karibuni imetwaa ubingwa wa kombe la Mapinduzi, lakini wakasema hilo haliwapi wasiwasi kwani tayari wamejiandaa kukabiliana na timu kubwa na walifanya hivyo kwa Azam na leo ni zamu ya Simba hivyo imewataka mashabiki wakje kujitokeza kwa wingi kushuhudia soka la vijana wao dhidi ya mnyama Simba.