Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Equatorial Guinea walenga Kombe la Dunia

Esteban Becker

Kocha mwenye ndoto kubwa wa wenyeji wa Kombe la Mataifa ya Afrika, Equatorial Guinea, Esteban Becker amehimiza vijana wake watumie dimba hilo kama ngazi ya kufuzu Kombe la Dunia.

Becker wa kutoka Argentina ambaye alichukua utawala wa Nzalang Nacional mapema mwezi huu, amekuwa na majuma mawili pekee kuandaa kikosi chake kujitosa uwanjani nyumbani wakati shindano hilo litakapongoa nanga Jumamosi dhidi ya Congo Brazzaville jijini Bata kwenye Kundi A.

Ingawa kufuzu robo fainali ya awamu ya 2012 wakati nchi hiyo iliandaa kwa pamoja na Gabon ni lengo mufti, Becker anatizama mbele zaidi na azima yake ya kuwaongoza kuingia Kombe la Dunia kwa mara ya kwanza kwenye historia yao.

“Naota kila wakati kushiriki Kombe la Dunia kwa hivyo bidii zangu zote zitaelekezwa kutayarisha kikosi chetu changa kuwa na nafasi ya kuwania tiketi ya kucheza dimba hilo lijalo la 2018,” Becker ambaye aliongoza kikosi cha taifa cha wanadada cha taifa hilo kinyakua ubingwa wa Afrika miaka mitatu iliyopita aliongeza.


Equatorial Guinea wanashiriki dimba la Mataifa kufuatia kujiondoa kwa Morocco kama wenyeji Novemba iliyopita na utawala wa taifa hilo ndogo kukubali mwito wa shirikisho la kandanda la Afrika CAF kuchukua mahala pao kama wenyeji wa dharura.

“Tuna wachezaji wenye uzoefu (Javier) Balboa na Juvenal (Edjogo-Owono) na chipukizi ambao wanachezea vilabu vizuri Uhispania kama Mallora, Malaga na Valencia.
“Tumekusanya pamoja kundi la wachezaji wenye ari kwa siku kumi pekee, kimawazo, wana nguvu za kustahimili na wameimarika na mbinu,” aliongeza.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FIFA yatoa orodha ya vilabu bora duniani, Simba na Yanga zachuana vikali

SHIRIKISHO la Soka Afrika (CAF) limetoa orodha ya viwango vya ubora wa klabu barani, Simba ikiendelea kuwa juu ya klabu nyingine za Tanzania, nafasi ya tano. Orodha hiyo imetoka leo kuelekea droo ya hatua za awali za michuano ya klabu Afrika ambayo kwa mara ya kwanza kihistoria itafanyika nchini katika studio za Azam Tv, Tabata Jijini Dar es Salaam. Yanga ambayo kama Simba itashiriki Ligi ya Mabingwa — yenyewe inashika nafasi ya 12, wakati timu nyingine katika orodha hiyo ni Namungo FC wanaoshika nafasi ya mwisho, ya 75 kwa pamoja na Salitas FC ya Burkina Faso, Ahli Benghazi ya Libya na NAPSA Stars ya Zambia. Kwa msimu ujao mbali na Simba na Yanga kushiriki Ligi ya Mabingwa, Azam FC na Singida Black Stars zitashiriki michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika.

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

Timu inaitwa Mashujaa Lake Tanganyika FC ( Mashujaa FC ) ilianza rasmi kampeni yake ya kupanda Ligi Kuu tarehe 29/9/2018 na imepanda Ligi Kuu 25/06/2023 miaka mitano ya kupambana kwenye Ligi Daraja la kwanza Championship. Timu hii inaendeshwa kwa ushirikiano wa pande mbili kati ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji kwa niaba ya Wananchi wa Kigoma. Muelewe hapa maana wengi wanasema ni timu ya Jeshi asilimia 100% Nembo ya timu ni Sokwe Dume, Shujaa wa Hifadhi za Gombe na Mahale zilizopo mkoani Kigoma. Rangi ya kwanza ya jezi ya timu (first kit) ni hiyo hapo chini na kwenye nembo ya timu ni rangi za tunda la michikichi (mawese ). Hii kama njano ni mawese yaliyoganda na huo wekundu ni mawese ya moto. Ukishika tunda la Mse juu utaona wekundu na ukikata katikati utaona njano. Nyeupe ni ‘nazi’ ya Mse hizi ni alama za utajiri wa Kigoma Jezi nyingine ni blue inayowakilisha Ziwa Tanganyika na Jezi nyingine ni Nyeupe

Beno Ngassa mdogo wa Mrisho Ngassa anayekipiga Tanzania Prisons

Miongoni mwa viungo wa pembeni wanaofanya vizuri ni Benodict Khalfan Ngassa ambaye amekuwa akifanya vizuri. Ngassa ambaye ni mtoto wa mchezaji wa zamani wa Pamba Jiji na Simba SC, Khalfan Ngassa, pia ni mdogo wa kiungo mshambuliaji wa zamani wa Yanga, Simba na Azam, Mrisho Ngassa anatajwa ni mmoja kati ya wachezaji wanaotazamiwa kufanya makubwa siku za usoni. Mambo Uwanjani Blog itawaletea Makala maalum ya kiungo huyo hatari ambaye ndoto zake ni kufuata nyayo za kaka yake Mrisho Ngassa. Beno Ngassa