GRANT NUSURA AMTIMUE AYEW

Dede Ayew 

Avram Grant alikuwa nusura amtimue kiungo wa kati kutoka wa Ghana Andre Ayew kutoka kwa kambi ya timu hiyo nchini Uhispania.

Kisa hicho, kilichofanyika wiki jana, kilipelekea bosi huyo wa Ghana wa miaka 59 kuanzisha shughuli ya kumfukuza mchezaji huyo kutoka Seville baada ya nyota huyo wa klabu ya Marseille kufika kambini akiwa amechelewa.
Lakini naibu mwenyekiti wa kamati simamizi ya Black Stars, Kudjoe Fianoo, aliingilia kati na kumsihi kubadilisha uamuzi wake.

“Mimi na [mwenyekiti wa kamati] George Afriyie tulilazimika kuingilia kati na kuomba radhi kwa niaba ya Andre Ayew kwa kufika kambini akiwa amechelewa kwa sababu Avram Grant alikuwa amekasirishwa sana na mchezaji huyo kufika Uhispania akwia amechelewa,” afisa huyo aliambia Happy FM mjini Accra.


Fianoo akaendelea: “Grant anamuona Dede kama mchezaji anayeweza kuongoza timu hii siku za usoni na anamtaka kuishi maisha ya kuigwa.”

Mashabiki wa timu hiyo ya taifa wametaka kiboko kitumiwe mara nyingi kuhakikisha nidhamu, hasa baada ya taifa hilo kulimbikiza sifa mbaya fainali zilizopita za Kombe la Dunia.

Andre anadaiwa kueleza majuto yake na kutoa ufafanuzi kuhusu sababu zilizopelekea yeye kuchelewa.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA