Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Julai, 2016

AZAM YAMALIZANA NA MBAYA WA YANGA

Picha
Na Salum Fikiri Jr  DAR ES SALAAM KLABU bingwa Afrika mashariki na kati Azam FC imefanikiwa kumsainisha winga machachari wa Medeama ya Ghana Enock Atta Agyoi kwa mkataba wa miaka miwili. Atta alikuwa tishio kwa mabingwa wa soka Tanzania bara Yanga SC katika mchezo wa makundi kombe la Shirikisho dhidi ya Medeama, katika mchezo huo uliofanyika uwanja wa Taifa Dar es Salaam  Yanga ililazimishwa sare ya kufungana 1-1. Ina maana Ataa ataitumikia Azam FC msimu ujao na katika mchezo wa Ngao ya Hisani ambapo Azam itakutana na Yanga katika uwanja wa Taifa

SIMBA YAIBOMOA TENA AZAM

Picha
Na Mrisho Hassan, DAR ES SALAAM BAADA ya kufanikiwa kumsana mshambuliaji hatari Ally Ame 'Zungu', Klabu ya Simba imeendelea kuibomoa Azam, Na safari hii ikifanikiwa kumnasa mlinda mlango mahiri Mwadini Ally Mwadini ambaye pia ni kipa wa timu ya taifa ya Zanzibar, Zanzibar Heroes. Habari zenye uhakika kutoka ndani ya klabu hiyo zinasema kuwa, Mwadini amesainishwa mkataba wa miaka miwili na atakipiga kwenye klabu hiyo hadi mwaka 2018. Mwadini hakuwa na wakati mzuri alipokuwa Azam ambapo alikuwa akiwekwa benchi la kipa bora wa Ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara 2015/16 Aishi Manula, hata hivyo Mwadini asingeweza kurejea langoni kwani timu hiyo imemleta kipa wa kombe la Dunia raia wa Ivory Coast

SIMBA SASA YAMRUDISHA LOGARUSIC

Picha
Na Ikram Khamees, DAR ES SALAAM SIMBA SC sasa ni kama inamrudisha kocha wake wa zamani Mcroatia Zdravko Logarusic hasa baada ya kuipa mwaliko timu yake mpya ya Interclube ya Angola ambapo sasa itakuja kucheza na Simba katika tamasha la Simba Day katika uwanja wa Taifa Dar es Salaam. Awali Simba iliialika Gor Mahia ya Kenya lakini sasa imeamua kuialika Interclube ya Angola moja kati ya vilabu vikubwa nchini humo, Rais wa klabu ya Simba Evans Aveva amesema leo kwamba Simba itacheza na Interclube na itatambulisha kikosi chake chote. Aveva amedai mbali na kutambulisha  kikosi kipya, Simba pia itatambulisha jezi zake mpya itakazotumia kwenye Ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara, Simba itafungua na Ndanda FC 'Wana-Kuchele'

MO SASA KUKABIDHIWA TIMU JULAI 30

Picha
Na Saida Salum, DAR ES SALAAM UONGOZI wa klabu ya Simba umeonyesha nia ya kumkabidhi klabu hiyo mfanyabiashara maarufu nchini Mohamed Dewji "Mo". Mambo Uwanjani imezipata taarifa za ndani kabisa ambazo zinasema kwamba Mo anakabidhiwa timu hiyo Julai 30 mwaka huu ambapo kutafanyika mkutano mkuu wa wanachama. Katika mkutano huo, wanachama wa Simba wataamua wenyewe kama klabu yao iendeshwe kisasa yaani kampuni ama iendelee na mtindo uleule wa wanachama. Endapo Simba itachagua kuwa kampuni basi ni sawa kama wamempa klabu hiyo Mo ambaye ameonyesha nia kubwa ya kuinunua timu hiyo, Mo anataka kuinunua Simba kwa shilingi Bilioni 20 ni sawa na kuinunua Simba kwa asilimia 51 na hisa nyingine atawaachia Simba wenyewe

AMOSI KIPANDE, ANAYEJIANDAA KULIZIBA PENGO LA MR EBBO

Picha
Katika Burudani Leo Taunamzungumzia Mwahiphop Amosi Mkama A.K.A Boss Rapper Ama Kipande Na Wana. Msanii Pekee Ambaye Anaweza Kuliziba Pengo La Marehemu Mr Ebbo. Kutokana Na Mashaili Yake Mazuri Yenye Ujumbe Wa Kuchekesha Na Kufundisha. Ukweli Utabaki Kuwa Ukweli Pale Alipo Achia Nyimbo Yake Iitwayo Pesa Shobo. Aliyowashirikisha  Golo Man Na Moriento Katika studio Ya Hekiman Records Chini Ya Producer Galatone Money Na Meneja Sakaingo. Nyimbo Iliyo Mpa Mashabiki Wengi Sana Na Kujipatia Shoo Mbalimbali. Kwa Sasa Yuko Jikoni Akiipika nyimbo Yake Mpya Itwayo Shori Wa Kijiji. Amboyo Ameshindwa Kuniweka Wazi Atafanya Nanani, Amapekeyake Au Studio Gani. Aliniambia Ukuacheka Kama Kawaida Yake Akisema Uhusio Muda Wakuongea Kila Kitu Ila Mashabiki Wangu Wategemee Mambo Manzuri Kutoka Kwangu. Nimimi Mkola Man Kutoka Hale Ktk Habari Na Wasanii

WASANII WA BONGOFLEVA, BONGOMOVIE WAMLILIA JK

Picha
Na Mwandishi Wetu, DODOMA Wasanii wa Bongo Movie na muziki wa kizazi kipya wamesema watamkumbuka sana Mwenyekiti Mstaafu wa CCM, Jakaya Kikwete kwa msaada aliyowapatia kipindi cha utawala wake akiwa Rais na Mwenyekiti wa chama hicho. Wasanii hao wameyasema hayo mjini Dodoma walipofanya tamasha la Usiku wa Wasanii kwa ajili ya kumuaga baada ya kustaafu rasmi uwenyekiti wa chama hicho na kumuachia uongozi Rais John Magufuli. PICHA ZOTE NA EDWIN MJWAHUZI

WOLPER ALIPOAMUA KUREJEA CCM

Picha
Na Mwandishi Wetu, DODOMA MSANII maarufu wa filamu hapa nchini Jacquliene Wolper anayeunda kundi la Bongomovie hatimaye amerejea Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kuachana na swahiba wake Waziri mkuu aliyejiuzuru Edward Lowassa aliyejiunga na Chadema. Awali Wolper alijiunga Chadema na katika kampeni za Uchaguzi mkuu mwaka jana alikuwa mpiga debe namba moja wa Lowassa aliywgombea urais kupitia Chadema. Akiwa mjini Dodoma ulikofanyika mkutano mkuu wa CCM ambao ulihitimisha uenyekiti wa Rais mstaafu wa awamu ya nne Dk Jakaya Kikwete, Wolper na wengine walitangaza kurejea CCM na kudai upinzani ni sawa na kibudu. Pichani chini Wolper akionekana kufurahia kurejea CCM

YANGA WAAHIDI USHINDI KWA MEDEAMA

Picha
Na Salum Fikiri Jr, DAR ES SALAAM YANGA SC imeondoka leo kuelekea Ghana tayari kabisa kwa ajili ya mchezo wa marudiano dhidi ya Medeama, hatua ya makundi kombe la Shirikisho barani Afrika. Mabingwa hao wa bara na Ngao ya Hisani, wameondoka na wachezaji wao wote isipokuwa Vicent Bossou na Hassan Kessy, Akizungumza na mtandao huu, kocha wa Yanga Mholanzi Hans Van der Pluijm ameahidi ushindi katika mchezo huo. Awali Yanga ililazimishwa sare ya kufungana 1-1 katika uwanja wake wa nyumbani wa Taifa jijini Dar es Salaam hivyo itakuwa na kazi ya ziada ili angalau kuchomoza na ushindi ili kufufua matumaini ya kutinga Nusu fainali. Katika kundi A, Yanga inashika mkia ikiwa na pointi moja wakati TP Mazembe ya DRC inaongoza kwa kukusanya pointi 7, Mo Bejaia wana pointi 5, wakati Medeama wana pointi 2 tu

CHIDIABELE ARUDI STAND UNITED

Picha
Na Paskal Beatus, SHINYANGA MSHAMBULIAJI wa Coastal Union ya Tanga  Chidiabele Abaslimu amerejea kwenye timu yake ya zamani ya Stand United kwa mkataba wa miaka .miwili imefahamika. Chidiabele alikuwa na wakati mzuri alipokuwa Stand mwaka juzi lakini alipojiunga na Coastal Union makali yake yakapotea ghafla na kuiacha timu hiyo ikishuka daraja. Mshambuliaji raia wa Nigeria, alifunga mabao 10 wakati Saimon Msuva wa Yanga akiibuka mfungaji bora katika Ligi ya msimu wa 2014/15 ambapo Yanga SC ikatwaa ubingwa. Lakini msimu uliopita, Chidiabere hakuwa katika msimu mzuri na kujikuta akipotezwa na wenzake, mshambuliaji huyo alifunga bao moja licha ya kucheza mechi kadhaa

MICHANO: MIKE TEE: Ni sawa na mfugaji wa kuku wa kienyeji aliyekata tamaa baada ya kuku wote kufa kwa mdondo

Picha
Na Mkola Man, TANGA Yap Yap Yap Michano Leo Inamchana Mike T  Mnyalu. Mwana hip hop Aliye Fanikiwa Na Style Yake Ya Kinyalu. Alijipatia Mashabiki Wengi Sana, Hasa Ktk Nyimbo Zake Kama Sitobadilika Ft Q Chief, Nyalu Land Ft Lady Jay De, Nakupenda Ft Juma Nature, Utanipenda Ft Mad Ice. Leo Hii Namfananisha Na Mfugaji Wa Kuku Wa Kienyeji. Aliye Kata Tamaa Baada Ya Kuku Wake Kukumbwa Na Ugonjwa Wa Kideli Ama Mdondo. Kisha Akaamua Kuacha Ufugaji Akiamini Ufugaji Huwo Auna Faida Zaidi Ya Hasara. Kumbe Yeye Ndio Chazo Cha Hasara Ama Faida. Michano Inamshauli Mfugaji Asikate Tamaa, Ila Abadilishe Mfumo Wa Ufugaji Mabanda Yawe Masafi Hata Kama Niyakawaida Jingine Kinga. Micha Inawatakia Ijumaa Njema Nimimi Mkola Man Ktk Michano Ya Kujenga Na Walasikubomoa

NDANDA YAZIDI KUJIIMARISHA, YAMNASA TELELA

Picha
Na Salum Fikiri Jr, DAR ES SALAAM TIMU Ndanda ya Mtwara inayoshiriki Ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara, inazidi kujiimarisha katika usajili baada ya kufanikiwa kumnasa kiungo wa zamani wa Yanga, Salum Telela. Telela ambaye mkataba wake na Yanga uljmalizika, Na kocha wa Yanga Mdachi Hans Van der Pluijm alikataa kumuongezea mwingine, amejiunga na Ndanda kwa mkataba wa mwaka mmoja. Tayari Ndanda ilishafanikiwa kumnasa beki wa Simba Hassan Isihaka, kwa maana hiyo kikosi hicho cha Ndanda msimu ujao kitakuwa tishio, isitoshe Ndanda itafungua dimba kwa kucheza na Simba SC mchezo wa Ligi kuu bara

YANGA YAMZUIA PLUIJM

Picha
Na Saida Salum, DAR ES SALAAM UONGOZI wa Yanga SC umetangaza kumzuia kocha wake Mholanzi Hans Van der Pluijm kwamba hawezi kuondoka ndani ya klabu hiyo hata kama kuna timu imemuahidi donge nono. Yanga wamefikia maamuzi hayo kufuatia taarifa zinazoenezwa kwenye mitandao kwamba kocha huyo anatakiwa na timu moja ya barani ulaya. Pluijm ambaye ni mshindi wa tuzo ya kocha bora wa Tanzania, ameonekana kuzichachafya timu mbalimbali nchini na kufikia hatua ya kuionea gere Yanga ambayo imetwaa mataji yote makubwa nchini mwaka huu ikiwa chini yake. Tayari uongozi wa Yanga umefanikiwa kimbakisha kocha huyo kwa kumuongezea mkataba wa miaka miwili utakaomfanya asalie katika kikosi hicho hadi mwaka 2018

ANAYEKUMBUKWA: HABIBU MAHADHI, MFUNGAJI BORA LIGI KUU SAFARI LAGER 1998

Picha
Na Salum Fikiri Jr, DAR ES SALAAM ANATOKEA kwenye familia ya marehemu Omary Mahadhi bin Jabir kipa wa zamani wa African Sports, Simba SC na Taifa Stars, Habibu Mahadhi ni mtoto wa gwiji hilo la soka miaka ya 70 na 80. Habibu alitamba na Coastal Union ya Tanga akitumia guu la kushoto na aliibuka mfungaji bora wa Ligi kuu ya Safari Lager mwaka 1998 wakati huo ikichezwa kwa hatua ya makundi. Habibu aliyeanzia kwenye timu ya mtaani kwao Magomeni Kota ya Police Kids baadaye akajiunga na Big Bon ya Magomeni Mikumi timu aliyokaa nayo hadi aliporejea timu ya mtaani kwake ya Messina Linea. Big Bon iliyoanzia Ligi Daraja la nne ikapanda hadi Daraja la Tatu ngazi ya mkoa wa Dar es Salaam, kwa bahati mbaya timu hiyo ikavunjwa hasa baada ya aliyekuwa mfadhili wake Ahmed Bashwani kuachana na ufadhili. Mahadhi na wenzake wakaondoka na ndipo alipojiunga na Messina, Mahadhi na nyota mwenzake George Kavila wakaenda zao Coastal Union ya Tanga na katika msimu wake wa kwanza akaibuka mfungaji bora wa ...

MFUNGAJI BORA ZIMBABWE ATUA AZAM KUMRITHI BOCCO

Picha
Na Mrisho  Hassan, DAR ES SALAAM MSHAMBULIAJI anayeongoza kwa mabao Bruce Kangwa wa timu ya Ligi kuu nchini Zimbabwe ya Highlanders, amewasili nchinj leo tayari kabisa kujiunga na Azam FC inayonolewa na makocha raia wa Hispania. Kangwa ambaye pia ni mchezaji wa timu ya taifa ya Zimbabwe na anatoka kwenye klabu kongwe na kubwa nchini humo ametua leo akiwa tayari kurithi nafasi ya nahodha John Rafael Bocco ambaye ameshaonyeshwa mlango wa kutokea. Mshambuliaji huyo aliyetupia magoli 20 kwenye ligi ya nchi hiyo inasemekana ni mkali kuliko mshambuliaji wa Yanga Donald Ngoma ambaye naye ni raia wa Zimbabwe Bruce Kangwa akiwasili leo Airport

KIPUTE YANGA NA AZAM AGOSTI 17

Picha
Na Salum Fikiri Jr, DAR ES SALAAM MTIFUANO wa Ligi kuu bara unatarajia kuanza mwezi ujao, lakini kutakuwa na mchezo wa Ngao ya Hisani kati ya Yanga SC na Azam FC Uwanja wa Taifa Dar es Salaam. Mechi hiyo ya Ngao itakuwa ya nne kwa miamba hiyo huku mara zote Yanga ikitoka na ushindi, Ikumbukwe mwaka jana Yanga ilitwaa Ngao kwa kuifunga Azam kwa penalti 8-7 baada ya sare ya 1-1. Mara ya baada ya mechi hiyo ndipo Ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara itakapoanza, Je Yanga itaibuka na ushindi katika mchezo huo? au Azam watalipa kisasi! ngoja tuone

KIBADEN AONDOLEWA UKOCHA JKT RUVU

Picha
Na Saida Salum, DAR ES SALAAM TIMU ya JKT Ruvu imeamua kuachana na kocha wake mkuu Abdallah King Kibaden Mputa na kumpa mikoba hiyo mchezaji wa zamani wa Mlandege Malale Hamsini. Kibaden aliyekuwa akiinoa timu hiyo na kuikoa isishuke daraja, atakuwa mkurugenzi wa ufundi na atakuwa akidili zaidi na timu za vijana, kwa mujibu wa mtoa taarifa hizi anasema kuwa Malale Hamsini ataweza kukinoa kikosi hicho na kufanya vizuri msimu ujao. Kibaden pia amewahi kuzinoa Simba, Manyema, Ashanti, Kagera Sugar na timu ya taifa, Taifa Stars

IVO MAPUNDA ATUA AFC LEOPARDS

Picha
Na Prince Hoza, DAR ES SALAAM KIPA wa zamani wa Yanga, Simba na Azam, Ivo Philip Mapunda anakaribia kujiunga na timu ya AFC Leopards ya Kenya inayoshiriki Ligi kuu ya nchi hiyo (KPL). Akizungumzia usajili wake AFC, Mapunda amesema, Ligi ya Kenya imekuwa na neema kwake kwani kujiunga na timu hiyo kubwa nchini humo ni faraja kwake. Anasema AFC na Gor ni sawa na Simba na Yanga hivyo anajisikia furaha kucheza kwenye vilabu vikubwa katika ukanda huu, Mapunda alitemwa na Simba wakati wa usajili wa dirisha dogo, akajiunga na Azam ambayo nayo imetangaza kumtema

BOCCO AKATALIWA NA WAZUNGU AZAM

Na Mrisho Hassan, DAR ES SALAAM NAHODHA na mshambuliaji wa Azam FC, John Raphael Bocco "Adebayor" amekataliwa na makocha wapya wa timu kutoka Hispania. Bocco amekataliwa na makocha hao wakidai hana kiwango cha kuichezea timu hiyo chini yao, wakati Bocco akikataliwa, viongozi wa timu hiyo wanahaha kutaka kumuombea abakishwe lakini wazungu wamemgomea kabisa. Jonas Garcia raia wa Hispania na mwenzake Zeben Hainendez wamemtosa mshambuliaji huyo aliyewahi kuwa mfungaji bora wa Ligi kuu bara, Bocco ni mmoja kati ya washambuliaji tegemeo lakini wazungu wanasema hana lolote na hakustahili kucheza Azam na ndio maana timu hiyo haina mafanikio

MEDEAMA WAONDOKA NA YONDANI

Picha
Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM UONGOZI wa timu ya Medeama ya Ghana ambayo iliwakazia Yanga na kuilazimisha sare ya kufungana bao 1-1 mchezo wa kombe la Shirikisho barani Afrika hatua ya makundi Uwanja wa Taifa Dar es Salaam, wameondoka na jina la beki wa Yanga Kevin Yondani. Taarifa zenye uhakika kutoka kwe ye benchi la ufundi la timu hiyo zinasema Kevin Yondani amewavutia mno vigogo wa timu hiyo na wako radhi kuimwagia fedha yoyote watakayoitaka Yanga ili waweze kumnasa. Yondani alicheza vizuri katika mchezo huo ambao uliiwezesha Yanga kupata moja tangu waanze michuano hiyo, Yanga na Medeama watarudiana Julai 26 mwaka huu huko Ghana, matumaini kwa Yanga kusonga mbele bado yapo kwani inahitaji ushindi katika mchezo huo

CHANONGO ASAINI MIAKA MIWILI MTIBWA SUGAR

Picha
Na Ikram Khamees, MOROGORO KIUNGO mshambuliaji wa zamani wa Simba SC na Stand United, Haroun Chanongo amesaini Mkataba wa miaka miwili kujiunga na Mtibwa Sugar ya Manungu Turiani mkoani Morogoro. Akizungumza na mtandao huu, Mkurugenzi wa Mtibwa Sugar Jamal Bayser amesema wameamua kunsaini Chanongo kutokana na umuhimu wake katika kikosi chao, Chanongo amekatisha mkataba wake na Stand kufuatia mgogoro ulioitokea timu hiyo iliyogawanyika makundi mawili. Awali Chanongo na mwenzake Abuu Ubwa wlaisaini mikataba mipya chini ya uongozi wa Stand Kampuni, lakini baadaye Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania TFF likairudisha timu hiyo chini ya uongozi wa wanachama kitendo kilichopelekea wachezaji hao kutupiwa virago

JUMA ABDUL AWA MCHEZAJI BORA VPL, YANGA WANG' ARA

Picha
Na Saida Salum, DAR ES SALAAM USIKU wa Julai 17, 2016 kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom ambayo ndiyo Wadhamini wakuu wa Ligi kuu ya soka Tanzania bara, walitangaza na kutoa tuzo 13 kwa wachezaji, refa na timu bora zilizofanya vizuri msimu wa 2015/16, Vodacom kwa kushirikiana na TFF wamefanikiwa kuchagua na kutoa zawadi kwa washindi wa tuzi hizo. LISTI YA WASHINDI WA TUZI NA ZAWADI MBALIMBALI Mchezaji bora wa Ligi kuu 2015/16 Juma Abdul wa Yanga Tsh Milioni 9,228,820. Mfungaji bora ni Amissi Tambwe wa Yanga Tsh Milioni 5,742,940. Mchezaji bora chipukizi ni Mohamed Hussein "Tshabalala" wa Simba Tsh Milioni 4. Golikipa bora ni Aishi Manula wa Azam FC Tsh Milioni 5,742,940. Kocha bora ni Hans Van der Pluijm wa Yanga Tsh Milioni 8. Timu yenye nidhamu bora ni Mtibwa Sugar Tsh Milioni 17,228,820. Bingwa wa Ligi kuu ni Yanga Tsh Milioni 81,345,723. Mshindi wa pili ni Azam FC Tsh Milioni 40,672,861. Mshindi wa tatu ni Simba SC Tsh Milioni 29,052,044. Mshindi wa nne ni ...

SAMATTA ALIZWA DAR

Picha
Na Mrisho Hassan, DAR ES SALAAM BABA mzazi wa mshambuliajj wa kimataifa wa Tanzania Mbwana Samatta, mzee Ali Samatta amesikitikia kitendo cha baadhi ya watu kutumia jina la mwanaye Mbwana Samatta na kujinufaisha pasipo ridhaa yake mwenyewe. Akizungumzia hilo hivi karibuni, mzee Samatta ambaye mwanaye Mbwana anakipiga Genk ya Ubelgiji, amelalamika kuwa kuna baadhi ya watu wameandika jina la mtoto wake kwenye miradi yao ya biashara wakati kufanya hivyo ni kosa. "Ilipaswa wamshirikishe Samatta au familia yake, kuna baadhi ya mabasi yameandikwa Samatta pamoja na kubandika picha yake kubwa, pia yapo naadhi ya maduka yanatumia jina la Samatta, tutaanzisha msako mkali na tutakayemkuta anaendelea kutumia jina la mwanangu tutamkuchukulia hatua za kisheria", alisema

NGASSA AANZA MAISHA MAPYA MOROKA SWALLORS

Picha
Na Mwandishi Wetu, Afrika Kusini MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania Mrisho Ngassa hatimaye ameanza maisha mapya katika klabu yake mpya ya Moroka Swallors hasa baada ya klabu yake ya hapo mwanzo ya Free State Stars kupigwa bei. Ngassa aliyekuwa akiichezea Free State iliyomnunua kwa mkataba wa miaka mitano akitokea Yanga SC ya Tanzania amejikuta akiachana na timu hiyo baada ya kununuliwa na Moroka Swallors timu iliyoshiriki Ligi daraja la pili. Hata hivyo sasa Moroka itashiriki Ligi kuu ya ABSA ikichukua nafasi ya Free State, Ngassa na wenzake wamejumuhishwa kwenye kikosi hicho ina maana anakuwa mchezaji mpya wa Moroka Swallors ambayo iliwahi kutikisa katika miaka ya 90

YANGA YABANWA NA MEDEAMA NYUMBANI

Picha
Na Salum Fikiri  Jr, DAR ES SALAAM MEDEAMA ya Ghana jioni ya leo imeilazimisha sare ya kufungana bao 1-1 Yanga SC ya Tanzania mchezo wa kombe la Shirikisho barani Afrika uliofanyika uwanja wa Taifa Dar es Salaam. Yanga walikuwa wa kwanza kupata bao la mapema dakika ya kwanza kipindj cha kwanza likifungwa na mshambuliaji wake hatari Mzimbabwe Donald Ngoma, Lakini Medeama walisawazisha katika kipindi hicho cha kwanza na kuwa sare. Matokeo hayo yalibaki hivyo hadi mwisho wa mchezo licha ya mwamuzi kuongeza dakika tano za nyongeza, Kwa matokeo hayo Yanga sasa imepoteza matumaini ya kusonga mbele kwani ina pointi moja wakati Medeama wana pointi mbili na TP Mazembe wanabaki kileleni na pointi zao sita na Mo Bejaia wana pointi nne, Yanga watarudiana na Medeama Julai 26

MKOLA MAN ASEMA YEYE SI FREEMASON

Picha
Na Mwandishi Wetu, TANGA MSANII wa muziki wa kizazi kipya nchini Christopher Mhenga A K A Mkola Man amesema kuwa yeye si muumin wa freemason kama watu wanavyodhani na amewataka wale wote wanaomdhania wasifanye hivyo. Mkola Man anayetamba na wimbo wake mpya uitwao 'Kitabu cha historia', amedai kuna watu wanamuogopa wakidhani freemaso , pia anakosa ushirikiano kutoka kwa watu mbalimbali kutokana na imani hiyo iliyoota mizizi kwake. Msanii huyo mwenye maskani yake Hale mkoani Tanga, ameongeza kuwa kuna watu wanampigia simu kutaka waunganishwe kwenye imani hiyo lakini yeye hausiani kabisa na mtandao huo na wala hajui walipo, "Mimi sio freemason na wala siwajui walipo nashangaa kuhusishwa na freemason", alisema. Aidha msanii huyo amedai yupo mbioni kutengeneza video ya wimbo wake mpya wa Malavidavi Time aliourekodi jijini Dar es Salaam mwanzoni mwa mwaka huu

MANARA AISHUKURU YANGA

Picha
Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM MKUU wa kitengo cha Mawasiliano na Habari wa Simba SC Haji Sunday Manara ameisifu klabu ya Yanga ambao ni mahasimu wao wa jadi. Akizungumza na mtandao huu kabla ya kukwea pipa kuelekea nchini India kufanyiwa matibabu ya jicho lake la upande wa kushoto ambalo limepoteza uwezo wa kuona, ameishukuru Yanga ambayo imemchangia baadhi ya fedha kwa ajili ya matibabu. Yanga kupitia kundi lake la mashabiki wamemchangia msemaji huyo wa Simba kiasi kisichopungua milioni 1, msemaji wa Yanga Jerry Muro ndiye aliyejitokeza na kumkabidhi kiasi hicho cha fedha

MICHANO: DOGO TANO AMEKWAMA KUTOKA KIMUZIKI

Picha
Na Mkola Man, TANGA Yap Yap Yap Michano Leo Iko Mkoani Morogoro Wilayani Kilombero Kwenye Mji Waifakara A.K.A Amekufa Mamba Kwenye Kijiji Cha Mngeta Alimaarufu Kwa Kilimo Cha Mpunga Ama Pepeta. Yap Bila Kupoteza Muda Michano Inamchana Edson Tumwandi maarufu kama Dogo Tano Ambaye Nimsanii Chipukizi Kwa Wale Wasiye Mjua Ila Ni Nyota Kwa Wale Wanao Mjua. Nyota Ya Msanii Dogo Tano Imeshindwa Kung'aa Kutokana Na Kufunikwa Na Mawingu Na Mawingu Hayo Ili Yatoke Inaitajika Abadilishe Mfumo Ama ajitambue True Nichipukizi Asifanye Kazi Na Produza Chipukizi Nikama Sifuri Jumlisha Sifuri Kisha Asiimbe na kupeleka nyi.bo zake katika Radio Za Mikoani Ambazo Nyingi Ni Chipukizi Na Madijei wake Pia Ni Chipukizi. Pia anaweza Kupata Meneja Chipukizi Najua Unakipaji Ila Kimezama Kwenye Maji Je! Ninuksi Ama Kimekamatwa Na Chunusi Pia Najua Na Kuchokoza Kwafaida Ili Upate Hasira Ili Uwekama Pweza Ilinikuvue Na Amini Katika Mafanikio Yako Utanikumbuka Daima Kwani Ukweli Nineno Lenye Uhai Basi Tukuta...

MKUDE ATIMKIA TENA SOUTH

Picha
Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM KIUNGO mkabaji na fundi Jonas Gerald Mkude ametimka tena katika kikosi cha Simba na kuelekea nchini Afrika Kusini kujaribu bahati yake nyingine ya kucheza soka la kulipwa. Taarifa ambazo zimethibitishwa zinasema kiungo huyo ameondoka Simba wiki iliyopita kuelekea Afrika Kusini kufanya majaribio ya kucheza soka la kulipwa katika klabu moja inayoshiriki Ligi kuu nchini humo. Hii ni mara ya pili kwa kiungo huyo mkabaji kwenda kufanya majaribio nchini Afrika Kusini, Awali alijiunga na Bidvest Wits lakini alishindwa, na sasa ameenda tena kujaribu bahati yake. Mchezaji huyo hakuwemo kwenye kikosi cha wachezaji 29 wa Simba walioingia kambini mjini Morogoro, Simba imeweka kambi Morogoro ikiwa tayari kabisa kujiandaa na msimu ujao wa Ligi kuu bara

YANGA WAAPA KUIANGAMIZA MEDEAMA

Picha
Na Shafih Shafih, DAR ES SALAAM KLABU bingwa ya soka Tanzania bara Dar Young Africans imewaahidi Watanzania iwe isiwe lazima wachomoze na ushindi itakapocheza na Medeama ya Ghana mchezo wa kombe la Shirikisho barani Afrika. Yanga na Medeama watacheza Jumamosi katika Uwanja wa Taifa Dar es Salaam na kiingilio cha kuiona mechi hiyo ni shilingi 3000, Yanga inahitaji ushindi katika mchezo huo ili waweze kufufua matumaini yao ya kutinga Nusu fainali. Tayari mabingwa hao wa bara, wamepoteza mechi mbili za mwanzo katika kundi A ikianza kucheza ugenini huko Algeria, Yanga ilifungwa 1-0 na Mo Bejaia  pia ikafungwa tena 1-0 nyumbani na TP Mazembe, endapo itapata ushindi itafufua matumaini

HASSAN ISIHAKA ATUA NDANDA

Picha
Na Salum Fikiri Jr, DAR ES SALAAM Nahodha wa zamani wa Simba SC, Hassan Isihaka amekamilisha dili ya kujiunga na Ndanda FC ya Mtwara kwa ajili ya kuitumikia msimu ujao. Ndanda moja kati ya timu zinaxoshiriki Ligi kuu ya Tanzania bara imemsajili beki huyo wa kati aliyemaliza mkataba wake na kulikuwa na mpango wa kujiunga na Mbao FC ya Mwanza. Isihaka ameshindwana na Simba baada ya kuitumikia kwa misimu miwili, msimu uliopita beki huyo aliyefanikiwa kubeba kombe la Mapinduzi na Ujirani mwema, alikorofishana na kocha wa timu hiyo Jackson Mayanja raia wa Uganda

WAPINZANI WA YANGA KOMBE LA SHIRIKISHO KUTUA KESHO

Picha
Na Mrisho Hassan, DAR ES SALAAM WAPINZANI wa Yanga katika michuano ya kombe la Shirikisho barani Afrika, Medeama ya Ghana inatarajia kuwasili nchini kesho Alhamisi ambapo Jumamosi ijayo watakutana Uwanja wa Taifa Dar es Salaam. Timu hizo zinakutana katika raundi ya tatu na ya mwisho katika mzunguko wa kwanza huku zote zikipepesuka, Yanga wenyewe wanashikilia mkia wa kundi A wakiwa hawana pointi hata moja. Medeama nao wana pointi moja, hivyo mchezo wa Jumamosi unatarajia kuwa mkali na wa kusisimua kwa sababu kila timu inahitaji matokeo ili kujiweka katika mazingira mazuri ya kuendelea hatua ya Nusu fainali

KUIONA YANGA NA MEDEAMA BUKU TANO

Picha
Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM MCHEZO wa mwisho wa kundi A kombe la Shirikisho Afrika kati ya Yanga SC ya Tanzania na Medeama ya Ghana utakaofanyika uwanja wa Taifa Dar es Salaam hatimaye watu hawataingia bure kwani kiingilio kimetajwa. Viingilio vimetwajwa ambapo VIP A watalipa Tsh 30, 000 na VIP B watalipa Tsh 20, 000, jukwaa la Orange watalipa Tsh 10, 000 na mzunguko Tsh 5000. Yanga inahitaji ushindi katika mchezo huo ili ifufue matumaini ya kusonga mbele, mabingwa hao wa bara wameshapoteza mechi zao mbili dhidi ya Mo Bejaia ya Algeria na TP Mazembe ya DRC. Kikosi hicho cha Wanajangwani kinaendelea na mazoezi katika uwanja wa Boko veterani

PRINCE HOZA ATEULIWA BALOZI WA MAVAZI

Picha
Na Mwandishj Wetu, DAR ES SALAAM KAMPUNI ya upendezeshaji na mavazi ya Ndulumo Junior Decorative (NJD) ya jijini Dar es Salaam imemteua Mtendaji mkuu wa Mambo Uwanjani Blogspot Prince Hoza kuwa balozi wa kampuni hiyo kwa kipindi cha mwaka mmoja. Akizungumza leo na mtandao huu, Mkurugenzi wa NJD Group Elias Januari amesema kampuni yake imeamua kumteua Hoza kuwa balozi wao kutokana na kuridhishwa na utendaji wake hasa katika mbao za matangazo. "Hoza atatusaidia katika kuitangaza kampuni yetu kupitia blogu yake, Hoza pia ana kurasa yake katika gazeti la Msimbazi hivyo tumeona bora tufanye naye kazi", alisema Januari. Kwa sasa NJD wana T: Shirt zao zinazopatikana maeneo mbalimbali jijini Dar es Salaam na zikiuzwa kwa bei ya Tsh 15, 000 na 10, 000 zikiwa katika kiwango cha ubora wa juu, Naye Prince Hoza amefurahishwa na uteuzi huo akiamini atafanya kazj na kampuni hiyo, Hoza sasa atakuwa akiinadi kampuni hiyo nchi nzima. T Shirt zao zenye majina ya Usi4C Nikuamini na Be Disti...

MAONI: TFF WAMESAHAU MAJUKUMU YAO

Picha
Na Prince Hoza, DAR ES SALAAM KAZI kubwa inayotakiwa kufanywa na Shirikisho la mpira wa miguu nchini TFF kuendeleza soka hapa nchini, pia kazi yao nyingine ni kuhakikisha maadili yanakuwepo kwenye mchezo huo. Maadili yenyewe ni usimamizi bora, na haki kwa mashindano yote wanayosimamia, kwa bahati mbaya TFF ya sasa inaongozwa na rais wake Jamal Malinzi imeshibdwa kusimamia vyote hivyo. Malinzi ameshindwa kufuata nyayo za mtangulizi wake Leodegar Chila Tenga ambaye ameondoka TFF lakini bado anakumbukwa kutokana na mema yake aliyoyafanya. Malinzi ameshindwa kusimamia maadili ambapo inafikia watu wa ngazi ya chini wanashindwa kuwaheshimu viongozi wao, kwa mfano soka la Tanzania mwaka huu limegubikwa na kashfa ya rushwa ambapo Shirikisho hilo nalo limetajwa kuhusika. Likiwa tayari limeshawapa baadhi ya watu adhabu kubwa ikiwemo kuwafungia maisha makocha na viongozi wa timu, pia wapo baadhi ya wachezaji nao wameadhibiwa. Hii yote imetokana na uuzo uliopo ndani ya Shirikisho hilo la kan...

KAVUMBAGU, IVO MORAD WATEMWA AZAM FC

Picha
Na Mrisho Hassan, DAR ES SALAAM KLABU bingwa ya soka Afrika mashariki n kati Azam FC imetangaza kuwaacha wachezaji wake sita wakiwemo watatu wa kimataifa kwa madai ya kushuka viwango vyao. Azam imewaacha makipa Ivo Mapunda na Khalid Mahadhi ambao hawakuwa na nafasi katika kikosi hicho, Mapunda aliyesajiliwa mwanzoni mwa msimu uliopita akitokea Simba, alicheza mechi moja tu. Wengine walioachwa ni mabeki Racine Diof raia wa Senegar na Said Morad, pia imewaacha washambuliaji wake Didier Kavumbagu raia wa Burundi na Alan Wanga raia wa Kenya. Kutemwa kwa wachezaji hao kunahirahisishia klabu ya Simba kuwanasa Kavumbagu na Morad ambao ilikuwa ikiwahitaji kwa udi na uvumba, Morad pia anatakiwa na Mbeya City ya jijini Mbeya

BATAROKOTA WA KTMA AKAMATWA KWA UTUPAJI TAKA MOROGORO

Picha
Na Ikram Khamees, MOROGORO MSANII wa muziki wa asili ambaye mwaka 2014 aliingia kwenye kinyang' anyiro cha kuwania tuzo za Kilimanjaro Tanzania Music Award (KTMA)  na wimbo wake wa Kwejaga Nyangisha, Batarokota, juzi alikamatwa na mgambo wa manispaa wa mji wa Morogoro kwa kosa la kutupa taka. Kwa mujibu wa mwandishi wetu aliyeshuhudia tukio hilo, Batarokota alionekana akitupa chupa ya maji ndipo askari hao wa mgambo waliokuwa wakikatiza mitaani walipomuona na kumtia hatiani. Hata hivyo msanii huyo alishikiliwa kwa masaa mawili na kuachiwa baada ya kutetewa na mwenyekiti wa mtaa wa Nane Nane Bi Ruth Kipawa kumuombea msamaha na kuachiwa huku akitakiwa kuhamasisha wananchi wasitupe takataka hovyo kwani ni kosa kisheria

JUMA ABDUL, TSHABALALA, KICHUYA KUWANIA UCHEZAJI BORA VPL

Picha
Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM Hafla ya kukabidhi tuzo mbalimbali za washindi wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kwa msimu wa 2015/2016 itafanyika Julai 17 mwaka huu. Jumla ya tuzo 13 za Ligi hiyo inayodhaminiwa na kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania zitatolewa katika hafla hiyo itakayofanyika jijini Dar es Salaam, na kuratibiwa na Kamati ya Tuzo ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF). Kamati hiyo inaundwa na waandishi wa habari za michezo, makocha, viongozi  (administrators) na wawakilishi kutoka kwa wadhamini (Vodacom na Azam Tv). Tuzo hizo ni mabingwa, makamu bingwa, mshindi wa tatu, mshindi wa nne, timu yenye nidhamu, mfungaji bora, mchezaji bora wa Ligi, kipa bora, kocha bora, mchezaji bora chipukizi, mchezaji bora wa kigeni, goli bora la msimu na mwamuzi bora. Waliopendekezwa (nominees) kuwania tuzo ya mchezaji bora wa Ligi ni Shiza Kichuya (Mtibwa Sugar), Juma Abdul (Yanga) na Mohamed Hussein (Simba) wakati kwa upande wa kipa bora ni Aishi Manula (Aza...

MCHEZAJI WA SMALL SIMBA AFARIKI DUNIA

Picha
Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM MCHEZAJI wa zamani wa Small Simba ya Zanzibar na AFC ya Arusha Mossi Shaaban amefariki dunia baada ya kuugua maradhi ya Kisukari kwa muda mrefu. Kiungo wa zamani wa Mlandege na Yanga SC Deogratus Lucas ameitonya Mambo Uwanjani kwamba marehemu alikuwa akisumbuliwa na kisukari kwa muda mrefu na kusababisha akatwe mguu wake mmoja. Lucas amedai Mossi amefariki leo na mipango ya mazishi inapangwa na wanafamilia, mchezaji huyo amewahi kutamba na Small Simba timu ambayo ilikuwa ikitikisa soka la Zanzibar na Tanzania kwa ujumla

SHIZA KICHUYA AANGUKA SIMBA MIAKA MIWILI

Picha
Na Ikram Khamees, DAR ES SALAAM LICHA kwamba viongozi wa Simba wanafanya siri, Lakini taarifa zinavuja kwamba winga wa Mtibwa Sugar ya Morogoro Shiza Ramadhan Kichuya amesaini miaka miwili tayari kabisa kukipiga na Wanamsimbazi. Mtibwa Sugar jana ilifikia makubaliano na Simba na kumruhusu winga huyo teleza ambaye leo ametangazwa kuwania tuzo ya mwanasoka bora wa Tanzania. Kusajiliwa kwa Kichuya na klabu ya Simba kunaifanya Mtibwa Sugar iondokewe na wachezaji wake watatu ambao wote wanajiunga na Simba, wachezaji wengine waliohamia Simba ni Muzamil Yassin, Mohamed Ibrahim na Kichuya

STAA WETU: MATTEO ANTONY SIMON, MKOMBOZI WA YANGA ALIYEIBEBA KIMATAIFA

Picha
Na Prince Hoza, DAR ES SALAAM WENGI wanajua mashujaa wa Yanga ni Donald Ngoma, Amissi Tambwe na Thabani Kamusoko, Lakini wanashindwa kufahamu kwamba Yanga SC inaye shujaa ambaye si mwingine ni Matteo Antony Simon. Huyo ni mshambuliaji wa Yanga ambaye alisajiliwa mwanzoni mwa msimu uliopita akitokea KMKM ya Zanzibar, Matteo ilikuwa asajiliwe na Simba lakini kama unavyofahamu vigogo hao wa soka nchini wamekuwa na kawaida ya kunyang' anyana wachezaji. Hatimaye Matteo akatua Yanga ingawa hakuwashangaza mashabiki wa timu kwakuwa hakuwa maarufu, mshambuliaji huyo aliyeonekana msumbufu tangia akiwa na kikosi cha KMKM, hakuwa katika kikosi cha kwanza cha Yanga kinachonolewa na Mholanzi Hans Van der Pluijm. Matteo alikuwa akianzia benchi na hii yote inatokana na Yanga kuwa washambuliaji wengi ambao wamekuwa msaada mkubwa kwenye klabu hiyo ambayo msimu uliopita iliweza kukusanya vikombe vyote vikubwa hapa nchini. Yanga imeweza kuchukua Ngao ya Hisani ikiwafunga Azam FC kwa mikwaju ya penal...

MEXIME ATIMKIA KAGERA SUGAR

Picha
Na Ikram Khamees, DAR ES SALAAM KLABU ya Kagera Sugar ya Misenyi Bukoba mkoani Kagera imefanikisha kumnyakua kocha wa Mtibwa Sugar Mecky Mexime na kumtangaza kama kocha wake mkuu. Taarifa zenye uhakika zilizothibitishwa na mkurugenzi wa Kagera Sugar Mohamed Hussein amesema ni kweli timu yake imemsainisha Mexime na sasa atakuwa kocha mkuu wa Kagera Sugar  hata hivyo Mexime anarithi mikoba ya Adolf Rishard ambaye alikuwa kocha wa timu. Naye msemaji wa Mtibwa Sugar Tobias Kifaru amekiri kuondoka kwa Mexime lakini amedai yupo jijini Dar es Salaam wakitafuta eneo la kuweka kambi kwa ajili ya maandalizi ya msimu ujao, Mambo Uwanjani inafahamu kuwa Mtibwa Sugar iko katika mazungumzo ya mwisho na Salum Mayanga ili aje achukue nafasi ya Mexime, Mayanga alikuwa kocha wa Prisons

SIMBA YAMLETA RAFIKI WA MAJABVI

Picha
Na Salum Fikiri Jr  DAR ES SALAAM SIMBA SC imeanza harakati zake za kuimarisha kikosi chake baada ya kumleta beki kisiki anayedaiwa kuwa ni kiboko ya mshambuliaji hatari wa Yanga Donald Ngoma, Method Mwanjali raia wa Zimbabwe. Licha kwamba beki huyo kudaiwa ni mzee ana miaka 33 lakini ana uwezo mkubwa wa kusakata kandanda  Method ni chaguo la kiungo mwingine wa Simba anayedaiwa kutimkia Austria Justice Majabvi. Endapo beki huyo ambaye pia anacheza kama kiungo mkabaji, atachukua nafasi ya Paul Kiongera, Tayari Simba imeshafanikiwa kuwasajili wachezaji watano wa ndani na sasa imegeukia wa kigeni

MICHANO; MR CHEKA ALISAHAU KAMA KUCHEKA NA KULIA YOTE NI MAKELELE

Picha
Na Mkola Man, TANGA YAP....yap...yap.Michano ya leo inamchana msanii wa muziki wa bongofleva mkazi wa Dar es Salaam lakini mwenyeji wa mkoa wa Kilimanjaro anajulikana kwa jina la Anselin Malembo zamani alikuwa akijiita Ans B. Huyu jamaa alitoka na wimbo mmoja aliomshirikisha msanii wa TMK Wanaume Family Mheshimiwa Temba, wimbo huo uliitwa Mr cheka ambao ukatamba vilivyo. Jamaa baada ya kuona ametusua akaanza kujisahau na kucheka, akawa kama fisi aliyeona mzoga uliouawa na Simba badala ya kula na kuondoka zake kisha kujipanga na kutafuta wa kwake akaanza kucheka  kumbe kucheka na kulia yote ni makelele. Mr Cheka alijua muziki ule alioutoa umetamba kwa sababu yake  kumbe Mheshimiwa Temba ndio kaubeba ule wimbo na ndio maana akauweka katika albamu yake  Mr Cheka hivi karibuni katoa wimbo mpya unaitwa Nacheka. Kwa maono yangu jamaa amechemka kwani hakukuwa na umuhimu wa kutoa wimbo unaofanana na ule wa mwanzo na vilevile kushirikisha wasanii wenye majina kama Juma Nature...

JERRY MURO ALA KITANZI MWAKA MMOJA NA TFF

Picha
Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM KAMATI ya Nidhamu ya Shirikisho la kandanda nchini TFF leo limemtia hatiani Mkuu wa kitengo cha Habari na Mawasiliano wa klabu ya Yanga, Jerry Muro kutojihusisha na masuala ya mpira wa miguu kwa muda wa mwaka mmoja. Taarifa zilizopatikana kutoka TFF zinasema Muro atatumikia adhabu hiyo kuanzia leo na kesho TFF itaweka bayana kila kitu. Afisa wa Habari wa Shirikisho hilo Alfred Lucas amesema kesho watatangaza kilichotokea kwenye kikao cha leo kilichoamua masuala mbalimbali yanayowahusu wanamichezo, Mambo Uwanjani inafahamu kuwa Muro ameadhibiwa mwaka mmoja baada ya kusikika akiitunishia misuli TFF

KIPA WA ASEC MIMOSAS AJA KUMRITHI AISHI MANULA AZAM

Picha
Na Mrisho Hassan, DAR ES SALAAM KIPA raia wa Ivory Coast aliyepata kutamba na klabu ya Asec Mimosas, Daniel Yeboah Tetch amewasili nchini leo na atasaini mkataba wa kujiunga na timu hiyo kisha kuondoka zake. Hii ina maana atamrithi kipa wa timu hiyo Aishi Manula ambaye kwa kipindi chote alikuwa langoni peke yake pasipo kupata upinzani wowote wa namba. Yeboah kipa aliyepata kucheza kwenye timu ya taifa ya Ivory Coast iliyoshiriki fainali za kombe la dunia

MAMBO UWANJANI YAMPA TUZO YA UCHEZAJI BORA KAMUSOKO WA YANGA

Picha
Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM JARIDA la michezo la Mambo Uwanjani limempa tuzo ya uchezaji bora kiungo wa mabingwa wa soka Tanzania bara Yanga SC Thabani Michael Scara Kamusoko hasa baada ya kuzikonga mioyo ya watu. Mhariri wa jarida hilo Exipedito Mataruma amesema Kamusoko ni mchezaji bora wa Ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara baada ya kufanya vizuri kwa kipindi chote alichojiunga na timu hiyo. Kamusoko alijiunga na Yanga wakati wa usajili wa Dirisha dogo mwaka jana, alitua Jangwani akitokea timu ya FC Platinum ya Zimbabwe na ameshinda tuzo hiyo baada ya kuwabwaga Juma Abdul pia wa Yanga na Shiza Kichuya wa Mtibwa Sugar

ANAYEKUMBUKWA: EDIBILY JONAS LUNYAMILA: WINGA TELEZA YANGA SC

Picha
Na Prince Hoza, DAR ES SALAAM YANGA SC iliwahi kutamba katika michuano ya kombe la Kagame iliyofanyika nchini Uganda mwaka 1996 na Yanga wakawa mabingwa baada ya kuwachapa SC Villa mabao 3-1. Katika kikosi cha Yanga wakati huo walikuwa na winga wao machachari ambaye aliacha simulizi Uganda nzima, Edibily Lunyamila alitamba vilivyo kiasi kwamba wafanyabiashara nchini Uganda wakaanza kuandika mabango kwenye biashara zao yenye jina la winga huyo. Kwakweli alifunika vilivyo kwenye michuano hiyo, Lunyamila alitamba pia kwenye kikosi cha timu ya taifa, Taifa Stars, Lunyamila alijiunga na Yanga SC akitokea Biashara Shinyanga timu iliyoibukia kwenye ligi kuu ya Tanzania na ikapotea ghafla ikiacha simulizi. Lunyamila alitamba Yanga lakini baadaye ajaondoka baada ya kukorofishana na viongozi wa Yanga na akajiunga na Malindi ya Zanzibar kisha akasajiliwa na Simba SC ambapo alitamba nayo kabla hajaacha soka. Lakini kiungo huyo wa pembeni aliwahi kwenda kufanya majaribio ya kucheza soka la kul...

YANGA KUNUNUA NDEGE YAKE BINAFSI

Picha
Na Mrisho Hassan, DAR ES SALAAM KAMPUNI ya Quality Group inayomilikiwa na bilionea Yusuph Manji ambaye pia ni mwenyekiti wa mabingwa wa soka nchini Yanga SC imetangaza kuinunulia ndege pamoja na basi kubwa la kisasa klabu hiyo. Quality Group itafanya hivyo hivi karibuni hasa baada ya kuingia mkataba wa kuifadhili Yanga kufuatia kuvunjika kwa mkataba wao na TBL, Manji amesema Yanga itanunuliwa ndege yake binafsi ambayo itawasaidia kwa safari zao za hapa na pale. Hii itakuwa kwa mara ya kwanza kwa klabu ya soka hapa nchini kumiliki ndege yake binafsi, na endapo Yanga itanunua ndege italingana na TP Mazembe ya DRC inayomilikiwa na bilionea Moise Katumbi