Barker amtaka Okello
Kocha wa Simba SC, Steve Barker, anatajwa kuhitaji saini ya kiungo mshambuliaji wa Uganda, Allan Okello (26), anayekipiga katika klabu ya AS FAR Rabat ya Morocco, ili aje kuimarisha kikosi chake katika dirisha dogo la usajili. Okello ni jina linalofahamika vizuri katika soka la Tanzania, baada ya kuitumikia Yanga SC msimu uliopita. Katika kipindi chake pale Jangwani, Okello alionyesha kiwango bora sana, akiwa miongoni mwa wachezaji muhimu zaidi katika kikosi cha Wananchi. Uwezo wake wa kutengeneza nafasi, kupiga pasi za mwisho na kufunga mabao muhimu ulimfanya apendwe sana na mashabiki wa Yanga na kuwa mmoja wa viungo bora zaidi katika Ligi Kuu. Hata hivyo, safari yake ya kwenda Morocco haikwenda kama ilivyotarajiwa. Tangu ajiunge na AS FAR Rabat akitokea Yanga, Okello bado hajapata nafasi ya kupata namba katika kikosi cha kwanza. Hali hiyo imemfanya akose muda wa kucheza mara kwa mara na kushindwa kuonyesha kiwango chake cha kweli. Kwa mchezaji wa kiwango chake, kukosa nafasi ni jambo...