Simba yaridhia Msimu kuondoka
Ofisa Habari wa Simba SC, Ahmed Ally, amethibitisha kuwa klabu hiyo imemruhusu rasmi mchezaji wao kijana na chipukizi anayekipiga ndani ya kikosi cha Mnyama, Bakari Msimu, kwenda nje ya nchi kufanya majaribio ya soka la kulipwa.
Msimbazi wameamua kumfungulia milango na kumpa nafasi adhimu kijana huyo kwenda kupambania ndoto zake na kuonyesha kipaji chake kwenye anga za kimataifa, huku mashabiki wakisubiri kwa hamu kuona kama atafanikiwa kutoboa.
