Fadlu avunja ukimya, awajia juu waandishi
Kocha mkuu wa Young Africans, Fadlu Davids, amevunja ukimya kuhusu sakata lake na aliyekuwa klabu yake ya zamani, Simba SC, pamoja na baadhi ya vyombo vya habari vinavyomkosoa tangu kurejea kwake nchini Tanzania.
Akizungumza kuhusu namna alivyopokelewa na mashabiki wa soka pamoja na changamoto alizokutana nazo baada ya kujiunga na Yanga, Fadlu amesema:
“Kwanza, nimerudi Tanzania nikiwa na mbinu mpya tena kwa wapinzani wangu. Hili si jambo zuri kwao, kwa maana kila mtu anakuchukulia kama mtu ambaye amekuja kusoma mchezo wa klabu ya mpinzani.
“Nafikiri hilo ni jambo la kawaida unapohamia katika klabu ambayo hapo awali ilikuwa mpinzani wako, au unapokuwa umewahi kufundisha timu pinzani.
“Kuna jambo moja ambalo nimeliona. Nilipokuwa katika klabu nyingine, kulikuwa na kundi fulani la waandishi wa habari.
“Sasa nilipokuja Young Africans, nimekutana na kundi tofauti la waandishi wa habari.
“Bila shaka, baadhi ya waandishi wana mahusiano au ukaribu na klabu fulani, wengine hawana upande wowote, na wengine wana ukaribu zaidi na klabu yetu.
“Kama nilivyosema, ushindi ndiyo lugha ambayo kila mtu anaielewa. Hilo ndilo tunalopaswa kuendelea kulifanya.
“Tunataka kuweka alama yetu katika soka la Afrika na kuifanya Yanga ianze kutawala, hatimaye kuwa miongoni mwa miamba ya soka barani Afrika.”
