Machapisho

Zulfa Macho aingia fainali ya ndondi Afrika

Picha
Nahodha wa timu ya ngumi ya Taifa ya Tanzania kwa upande wa wanawake Zulfa Macho ameingia hatua ya fainali ya michuano ya ngumi barani Afrika inayofanyika nchini Kenya. Macho amemtandika kwa 'points' 5-0 mpinzani wake bondia kutoka nchini DR Congo, Deborah Bawo katika mashindano hayo ya kanda ya tatu yanayoendelea jijini Nairobi katika uwanja wa ndani wa Kasarani.

Azam FC yawaiga Yanga, kuingiza mashabiki bure dhidi ya KMKM

Picha
KLABU ya Azam FC imeamua watazamaji wataingia bure katika mchezo wa marudiano Raundi ya Pili ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya KMKM ya Zanzibar Ijumaa Uwanjan wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam. Baada ya ushindi wa 2-0 kwenye mchezo wa kwanza Ijumaa iliyopita Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar – Azam FC watakuwa nazi ya kulinda zaidi ushindi wa ugenini kwa kutokubakli kuruhusu baoi ili waende makundi.

TRA yashindwa kukusanya mapato kwa Mashujaa FC

Picha
TIMU ya TRA United, zamani Tabora United leo imelazimishwa sare ya bila mabao na jirani zao, Mashujaa FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora. Kwa matoke ohayo, TRA United inafikisha pointi tatu katika mchezo wa tatu baada ya awali pia kutoka sare ya 2-2 na Dodoma Jiji hapo hapo Mwinyi na 0-0 na wenyeji, Pamba Jiji FC Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza. Kwa upande wao Mashujaa FC wanafikisha pointi tano katika mchezo wa tano, nne za awali wakishinda moja, sare moja na kufungwa mbili. 

Twiga Stars yaigalagaza Ethiopia

Picha
TIMU ya taifa ya wanawake ya Tanzania, Twiga Stars imeibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Ethiopia katika mchezo wa kwanza Raundi ya Pili kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa Afrika Wanawake 2026 nchini Morocco jioni ya leo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es Salaam. Mabao ya Twiga Stars inayofundishwa na kocha Bakari Nyundo Shime yamefungwa na washambuliaji Aisha Juma Mnunka wa Simba Queens dakika ya 23 na Jamila Rajab Doxa wa JKT Queens dakika ya 56. Ethiopia inayofundishwa na Kocha Mkuu, Yosef Gebrewold itaikaribisha Tanzania Oktoba 28 katika mchezo wa marudiano Uwanja wa Abebe Bikila Jijini Addis Ababa kujaribu kupindua matokeo na mshindi wa jumla atafuzu WAFCON 2026 inayotarajiwa kuanza Machi 17 hadi April 3 mwakani. Twiga Stars imewahi kucheza Fainali za WAFCON mara mbili tu, 2010 nchini Afrika Kusini na 2024 nchini Morocco na mara zote wakitolewa katika hatua ya makundi.

Simba yatajwa kuwania tuzo ya klabu bora Afrika

Picha
Klabu ya Simba SC imetajwa kwenye orodha ya vilabu vinavyowania tuzo ya Klabu Bora ya Mwaka 2025 kwenye tuzo za CAF Awards zitakazotolewa mwishoni mwa mwaka huu.. Hizi ndizo klabu zilizotajwa: 🇩🇿 CR Belouizdad 🇩🇿 CS Constantine 🇨🇮 ASEC Mimosas 🇪🇬 Pyramids FC 🇲🇦 RS Berkane 🇿🇦 Mamelodi Sundowns 🇿🇦 Orlando Pirates 🇿🇦 Stellenbosch FC 🇸🇩 Al Hilal SC 🇹🇿 Simba SC 

Nabi kurejea Jangwani

Picha
Klabu ya Young Africans SC (Yanga) imeendelea kuwa kitovu cha mjadala katika anga la soka la Tanzania baada ya taarifa mpya kuibuka zikieleza uwezekano wa kurejea kwa kocha Nasreddine Nabi, aliyeiongoza timu hiyo katika kipindi cha mafanikio makubwa miaka michache iliyopita. Nguvu zimeelekezwa kwa Nabi, ambaye alileta mafanikio makubwa alipokuwa akiinoa klabu hiyo hadi kufika fainali ya Kombe la Shirikisho la CAF mwaka 2023. Mashabiki wengi wa Yanga wamepokea taarifa hizo kwa hisia kali, wengi wakiamini kuwa kurejea kwa Nabi kunaweza kuleta msisimko mpya ndani ya kikosi hicho. Wanamkumbuka kama kocha mwenye nidhamu, mbinu za kisasa na uwezo wa kushirikiana vyema na wachezaji wake.

Kapombe, Mayele kuwania tuzo CAF

Picha
Nahodha wa klabu ya Simba Sports Club ya Tanzania, Shomari Kapombe ametajwa kwenye orodha ya wachezaji 10 wanaowania tuzo ya mchezaji bora wa mwaka 2025 wa Shirikisho la soka Afrika CAF kwa wachezaji wa ndani inayowaniwa pia na mshambuliaji wa Pyramids Fc, Fiston Kalala Mayele. Ikumbukwe Kapombe ndie Mchezaji pekee kutoka Kusini mwa Jangwa la Sahara kupenya kwenye 10 bora huku Wachezaji wengine wote wakitokea Ligi za Morocco, Misri na Algeria. Wachezaji wengine wanaowania tuzo hiyo ni pamoja na mshambuliaji wa Al Ahli ya Libya, Ismail Belkacemi, kiungo wa Pyramids, lbrahim Blati Touré, aliyekuwa beki wa RS Berkane, Issoufou Dayo ambaye ametimkia Umm Salal Sc ya Qatar na winga Emam Ashour wa Al Ahly. Wengine ni aliyekuwa winga wa Pyramids, Ibrahim Adel ambaye ametimkia Al Jazeera Fc ya Saudi Arabia, nahodha wa AS FAR Rabat, Mohamed Hrimat, beki wa Pyramids,  Mohamed Chibi na mshambuliaji wa RS Berkane, Oussama Lamlioui.