KLABU ya Azam FC imeamua watazamaji wataingia bure katika mchezo wa marudiano Raundi ya Pili ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya KMKM ya Zanzibar Ijumaa Uwanjan wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
Baada ya ushindi wa 2-0 kwenye mchezo wa kwanza Ijumaa iliyopita Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar – Azam FC watakuwa nazi ya kulinda zaidi ushindi wa ugenini kwa kutokubakli kuruhusu baoi ili waende makundi.