Machapisho

Pyramid Football Club, Klabu changa nchini Misri na maajabu yake

Picha
Sio klabu kongwe kwenye soka la Africa na hata kwenye ligi kuu ya Egypt hawana historia kubwa ya mafanikio mwaka huu ndio kwanza wanatimiza miaka 17 baada ya kuanzishwa mwaka 2008. PYRAMIDS haijawahi kushinda kombe la ligi kuu ya Egypt hata mara moja imeishia tu nafasi ya pili(Runners) ndo mafanikio makubwa kwenye ligi kuu ya Egypt, Kwenye michuano ya CAF mafanikio makubwa ni final ya CAF confederation Cup msimu 2019/20. Kwenye CAF Champions league ndo wageni kabisa hawajawahi kufika stage kubwa kabisa kwanza hata kushiriki ilikuwa changamoto ila msimu huu wamefanya makubwa sana kuanzia kwenye ligi kuu hadi CAF Champions league ambapo wapo fainali. KRUNOSLAV JURCìC, kocha mkuu wa Pyramids ameingia kwenye rekodi ya klabu hiyo kwa kuipeleka Pyramid final ya CAF Champions league kwa mara ya kwanza kwenye historia ya klabu hiyo,Sajili za Pyramids za hivi karibuni zilionyesha nini klabu inataka hasa kwenye CAF tournament na sasa kila kitu kipo wazi timu ipo final. Uwekezaji mkubwa kwenye k...

Mayele aisogeza Pyramids fainali

Picha
Timu ya Pyramids ya Misri usiku huu imetinga fainali ya michuano ya Ligi ya mabingwa barani Afrika baada ya kuichapa Orlando Pirates ya Afrika Kusini mabao 3-2. Kwa matokeo hayo sasa Pyramids wanakwenda kukutana na Mamelodi Sundown's ambao mapema iliitoa Al Ahly kwa sheria baada ya sare ya 1-1 ugenini. Fiston Mayele nyota wa zamani wa Yanga ya Tanzania, leo ndiye shujaa baada ya kufunga mabao mawili, dakika ya 45 na 84 wakati bao lingine likifungwa na Ramadhan Sobhi dakika ya 56, mabao ya Orlando yamefungwa na Relebohile Mofokeng dakika ya 41 na Mohau Nkota dakika ya 52. Wakati huo huo Fiston Mayele anaongoza kwa ufungaji Bora wa Ligi ya mabingwa akiwa amepachika mabao 6. .

Azam FC wapo sana kombe la Muungano

Picha
Bao lililofungwa na mlinzi Lusajo Mwaikenda limeiwezesha Azam FC kuibuka na ushindi wa bao 1-0 na kutinga nusu fainali ya kombe la Muungano dhidi ya KMKM uwanja wa Gombani, Pemba visiwani Zanzibar. Azam FC inakuwa timu ya kwanza kwa upande wa Tanzania bara kutinga nusu fainali baada ya Singida Black Stars na Coastal Union kutupwa nje

Goli la kujifunga la Yasser Mohamed laipeleka fainali Mamelodi Sundown's

Picha
Goli la kujifunga lililofungwa na Yasser Ibrahim dakika ya 89 limeizamisha Al Ahly na kutolewa kwenye hatua ya nusu fainali Ligi ya mabingwa barani Afrika kufuatia sare ya kufungana bao 1-1 kwenye ardhi ya nyumbani dhidi ya Mamelodi Sundown's ya Afrika Kusini. Al Ahly walijipatia bao la kuongoza kupitia Taher Mohamed dakika ya 24, sasa Mamelodi Sundown's wanatamgulia fainali wakisubiri mshindi kati ya Pyramids na Orlando Pirates mchezo unaopigwa muda huu.

Mac Muga ni wimbo wa kweli- Alikiba

Picha
Mac muga ni wimbo wenye alama ya tofauti kwa catalogue ya Alikiba ulitokana na story ya kweli ya mtu halisi anayeitwa Mac Muga kama jina la wimbo huo.Na hapa ameshea nasisi kuhusu story ya Mac Muga: "Nafiki ilikuwa mida ya saa tisa wakati naelekea mazoezini, nakumbuka ndo kipindi ambacho nilitakiwa nielekee Yanga. Wakati nilipofika karibu na uwanja wa mazoezi ndipo nilipokutana na Mac Muga huku akiwa amejiinamia nikawa nimeuliza nini haswa kinamsibu, ndipo alipoanza kunisimulia story yake. na hapo nikapata wazo la wimbo wa Mag Muga.Alisema Alikiba Alikiba

Watakaomzika Papa Francis watajwa, Trump ndani

Picha
Orodha ya Viongozi wa dunia watakaohudhuria mazishi ya Papa Francis kesho Jumamosi ,Jijini Roma,Italia. António Guterres – Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ursula von der Leyen – Rais wa Kamisheni ya Umoja wa Ulaya António Costa – Rais wa Baraza la Ulaya Roberta Metsola – Rais wa Bunge la Ulaya Austria - Rais Alexander Van der Bellen Kansela Christian Stocker Ubelgiji - Mfalme Philippe, Malkia Mathilde Waziri Mkuu Bart De Wever Bulgaria - Waziri Mkuu Rossen Jeliazkov Croatia - Rais Zoran Milanović Waziri Mkuu Andrej Plenković Jamhuri ya Czech - Waziri Mkuu Petr Fiala Denmark - Malkia Mary Finland - Rais Alexander Stubb Ufaransa - Rais Emmanuel Macron Ujerumani - Rais Frank-Walter Steinmeier Kansela Olaf Scholz Ugiriki - Waziri Mkuu Kyriakos Mitsotakis Hungary - Rais Tamas Sulyok Waziri Mkuu Viktor Orbán Ireland - Rais Michael D. Higgins Waziri Mkuu Micheál Martin Naibu Waziri Mkuu Simon Harris Italia - Waziri Mkuu Giorgia Meloni Latvia - Rais Edgars Rinkēvičs Lithuania - Rais Gitanas Na...

Timu za bara mdebwedo Zanzibar, Coastal Union yatupwa nje kombe la Muungano

Picha
TIMU ya Zimamoto imefanikiwa kutinga Nusu Fainali ya Kombe la Muungano baada ya ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Coastao Union ya Tanga jioni ya leo Uwanja wa Gombani, Pemba. Pongezi kwa mfungaji wa bao hilo pekee, Rashid Salum dakika ya 28 na sasa wanaungana na ndugu zao, JKU waliokuwa wa kwanza kutinga Nusu Fainali jana jioni kwa ushindi wa penalti 6-5 kufuatia sare ya 2-2 ndani ya dakika ya 90 hapo hapo Uwanja wa Gombani, Pemba. Baadaye kuanzia Saa 1:15 usiku wa leo KMKM watacheza Azam FC ya Dar es Salaam katika Robo Fainali ya tatu ya michuano hiyo usiku hapo hapo Uwanja wa Gombani.