Timu ya Pyramids ya Misri usiku huu imetinga fainali ya michuano ya Ligi ya mabingwa barani Afrika baada ya kuichapa Orlando Pirates ya Afrika Kusini mabao 3-2.
Kwa matokeo hayo sasa Pyramids wanakwenda kukutana na Mamelodi Sundown's ambao mapema iliitoa Al Ahly kwa sheria baada ya sare ya 1-1 ugenini.
Fiston Mayele nyota wa zamani wa Yanga ya Tanzania, leo ndiye shujaa baada ya kufunga mabao mawili, dakika ya 45 na 84 wakati bao lingine likifungwa na Ramadhan Sobhi dakika ya 56, mabao ya Orlando yamefungwa na Relebohile Mofokeng dakika ya 41 na Mohau Nkota dakika ya 52.
Wakati huo huo Fiston Mayele anaongoza kwa ufungaji Bora wa Ligi ya mabingwa akiwa amepachika mabao 6.
.
