Sio klabu kongwe kwenye soka la Africa na hata kwenye ligi kuu ya Egypt hawana historia kubwa ya mafanikio mwaka huu ndio kwanza wanatimiza miaka 17 baada ya kuanzishwa mwaka 2008.
PYRAMIDS haijawahi kushinda kombe la ligi kuu ya Egypt hata mara moja imeishia tu nafasi ya pili(Runners) ndo mafanikio makubwa kwenye ligi kuu ya Egypt, Kwenye michuano ya CAF mafanikio makubwa ni final ya CAF confederation Cup msimu 2019/20.
Kwenye CAF Champions league ndo wageni kabisa hawajawahi kufika stage kubwa kabisa kwanza hata kushiriki ilikuwa changamoto ila msimu huu wamefanya makubwa sana kuanzia kwenye ligi kuu hadi CAF Champions league ambapo wapo fainali.
KRUNOSLAV JURCìC, kocha mkuu wa Pyramids ameingia kwenye rekodi ya klabu hiyo kwa kuipeleka Pyramid final ya CAF Champions league kwa mara ya kwanza kwenye historia ya klabu hiyo,Sajili za Pyramids za hivi karibuni zilionyesha nini klabu inataka hasa kwenye CAF tournament na sasa kila kitu kipo wazi timu ipo final.
Uwekezaji mkubwa kwenye kikosi cha Pyramids wachezaji kama BLATI TOURE kutoka Burkina Faso amefanya makubwa sana kwenye kikosi uwepo wa FISTON KALALA MAYELE umeongeza nguvu kubwa kwenye safu ya ushambuliaji na uwepo wa nyota wengine kwenye kikosi kumeipa Pyramids nguvu ya kupambana na uwezo wa kushindana kwenye mashindano makubwa.
Lakini pia ongezeko la mchezaji Ramadan Sobhi kwenye kikosi cha Pyramids umeongeza chachu kubwa, Sobhi ni mshambuliaji aliyepata makuzi ya soka pale Al Ahly kabla ya kutimkia Stoke City, Huddersfield na badae kurudi Al Ahly kwa mkopo kisha kujiunga na Pyramids msimu wa 2020.
Alijiunga na Pyramids kwa dau la dola 2M huku akichukua mshahara wa dola 1.4M kwa mwezi, huu ni miongoni kati ya usajili ulioleta chachu na kuongeza nguvu kwenye kikosi cha Pyramids.
Nb: Kumbe inawezekana klabu kama Pyramids kutunisha msuli mbele ya klabu kubwa kama Al Ahly na Zamalek.
