Azam FC wapo sana kombe la Muungano
Bao lililofungwa na mlinzi Lusajo Mwaikenda limeiwezesha Azam FC kuibuka na ushindi wa bao 1-0 na kutinga nusu fainali ya kombe la Muungano dhidi ya KMKM uwanja wa Gombani, Pemba visiwani Zanzibar.
Azam FC inakuwa timu ya kwanza kwa upande wa Tanzania bara kutinga nusu fainali baada ya Singida Black Stars na Coastal Union kutupwa nje
