Timu za bara mdebwedo Zanzibar, Coastal Union yatupwa nje kombe la Muungano
TIMU ya Zimamoto imefanikiwa kutinga Nusu Fainali ya Kombe la Muungano baada ya ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Coastao Union ya Tanga jioni ya leo Uwanja wa Gombani, Pemba.
Pongezi kwa mfungaji wa bao hilo pekee, Rashid Salum dakika ya 28 na sasa wanaungana na ndugu zao, JKU waliokuwa wa kwanza kutinga Nusu Fainali jana jioni kwa ushindi wa penalti 6-5 kufuatia sare ya 2-2 ndani ya dakika ya 90 hapo hapo Uwanja wa Gombani, Pemba.
Baadaye kuanzia Saa 1:15 usiku wa leo KMKM watacheza Azam FC ya Dar es Salaam katika Robo Fainali ya tatu ya michuano hiyo usiku hapo hapo Uwanja wa Gombani.
