Machapisho

Makonda sasa kuitwa baba Keagan

Picha
Na Ikram Khamees. Dar es Salaam Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam mheshimiwa Poul Charles Makonda amemtunuku jina mwanaye la Keagan ili kudhihirisha napenzi yake kwa mkali wa soka Kevin Keagan. Makonsa na mkewe wamebahatika kupata mtoto wa kiume baada ya miaka miwili ya ndoa yao, kwa furaha aliyonayo ya kupata mtoto, mheshimiwa Makonda aliandika katika ukurasa wake wa Instragram akielezea kumshukuru kwake mwenyezi Mungu. Hata hivyo Makonda akaamua kumpachika jina mwanaye huyo wa kiume la Keagan ikidhihirisha mapenzi yake na mchezo wa soka, Mambo Uwanjani nayo inatoa salamu za pongezi kwa mkuu huyo wa mkoa kwa kupata mtoto

Yanga kujaribu tena kwa Gormahia

Picha
Na Salum Fikiri Jr. Dar es Salaam Wawakilishi pekee wa Tanzania katika michuano ya kimataifa, Yanga Sc jioni ya leo wanapeperusha bendera ya nchi itakaposhuka uwanjani kuvaana na wenyeji wao timu ya Gor Mahia ya Kenya mchezo wa kombe la Shirikisho barani Afrika kundi D. Yanga ilisafiri juzi kuelekea mjini Nairobi ikiwakosa wachezaji wake wawili Hassan Kessy na Kelvin Yondani ambao wamegoma kusafiri wakishinikiza kupewa mikataba mipya. Pia imewakosa wachezaji wake wapya watatu Mrisho Ngasa, Deus Kaseke na Heritier Makambo ambao usajili wao umechelewa kuwasilishwa CAF, katika mchezo wa leo Yanga inahitaji ushindi ama sare ili kujiweka katika mazingira mazuri ya kusonga mbele ingawa haipewi nafasi ya kushinda kutokana na ubora ilionao Gormahia

Yondani kurejea Msimbazi

Picha
Na Saida Salum. Dar es Salaam Tetesi zilizoenea mchana wa leo jijini Dar es Salaam zinamuhusu beki kisiki wa Yanga SC ambaye amegoma kusafiri na kikosi hicho jana kuelekea nchini Kenya ambapo kesho wanaumana na Gormahia, Kelvin Yondani inasemekana anajiunga na Simba. Taarifa ambazo mchana wa leo zilisambaa kwa kasi ni kwamba mlinzi huyo asiyechuja alionekana katikati ya jiji la Dar es Salaam zilipo ofisi za bilionea Mohamed Dewji "Mo Dewji" akiingia na kutoka huku akiwa amezungukwa na kundi kubwa la wapambe. Mambo Uwanjani imeshuhudia Yondani akizunguka mara kadhaa na imejiridhisha kuwa kuna mazungumzo yamefanywa kati ya Simba na beki huyo ambaye mkataba wake na Yanga umemalizika. Za udukuzi zimebaini kuwa beki huyo anaitoboa Simba shilingi milioni 50 za Kitanzania na anarejea tena nyumbani kwani kabla hajaenda Jangwani alikuwa mitaa ya Msimbazi

Ndikumana asema amefuata noti KMC

Picha
Na Asha Maliyaga. Dar es Salaam Mlinzi wa kimataifa wa Burundi, Yusuph Ndikumana amesema amejiunga na KMC ya Manispaa ya Kinondoni jijini Dar es Salaam baada ya kutangaziwa donge nono na amedai ataipambania timu hiyo ili kutwaa ubingwa wa Tanzania Bara. Akizungumza kwa njia ya simu kutoka nyumbani kwao Burundi jana, Ndikumana amesema kuwa KMC iliyopanda daraja msimu uliopita ameamua kujiunga nayo baada ya kuitwa na kocha wake wa zamani Etienne Ndayiragije ambaye ni Mburundi. Ndayiragije ambaye mwaka jana alikuwa akiinoa Mbao FC ya Mwanza ambayo Ndikumana naye alikuwa akiichezea, amedai kufurahishwa na maslahi mazuri ndani ya kikosi hicho

Tarimba, Sanga wazika tofauti zao sasa kusaidiana kuijenga Yanga

Picha
Na Ikram Khamees. Dar es Salaam Hatimaye ule mgogoro uliokuwepo kati ya kaimu mwenyekiti wa klabu ya Yanga, Clement Sanga na aliyekuwa mwenyekiti wa kamati ya mpito ya klabu hiyo Tarimba Abbas Tarimba wamezika tofauti zao leo na kuahidi kushirikiana pamoja ili kuijenga upya Yanga. Wawili hao wamefikia maamuzi hayo baada ya tawi la Yanga, Viva Young International kuwaweka meza moja na hatimaye kufikia muafaka leo katika ofisi za Tarimba Abbas zilizopo Osterbay. Tawi hilo lilianza kuzungumza na kila mmoja wao na hatimaye kuwakutanisha pamoja na kufikia muafaka, kuanzia sasa wawili hao wamekubaliana kufanya kazi pamoja na kuweka kando tofauti zao, Tarimba alijiuzuru nafasi yake ya kuongoza kamati ya mpito baada ya kuchukizwa na matamko ya Sanga aliyoyatoa katika mkutano wake na viongozi wa matawi

Kispoti

Picha
10 wa kigeni fundisho tosha kwa wazawa Na Prince Hoza RAIS wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dr John Pombe Magufuli amewaji kuhoji kiwango cha timu ya Simba SC ilipocheza na Kagera Sugar Mei 22 mwaka huu katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara. Magufuli alikuwa mgeni wa heshima akishujudia Simba ikichapwa bao 1-0 na vijana wa Kagera Sugar wa kutoka Bukoba mkoani Kagera, lengo la kuhudhuria mchezo huo kwa Rais Magufuli ni kukabidhi kikombe cha ubingwa wa Bara kwa Simba SC ambao walikuwa na rekodi ya kutopoteza mchezo kwenye ligi hiyo. Rais wa Shirikisho la mpira wa miguu nchini, TFF, Wallace Karia ndiye aliyemuomba Rais Magufuli kuwa mgeni wa heshima katika mchezo huo ili kukabidhi kikombe cha ubingwa wa Ligi Kuu Bara Simba SC na pia kukabidhi kikombe cha ubingwa wa mataifa Afrika mashariki na kati CECAFA Junior Challenge Cup kwa vijana chini ya miaka 17 Serengeti Boys ambao walishinda huko Kenya. Lakini Rais Magufuli alishuhudia kiwa...

Adam Salamba apata ajali, anusurika

Picha
Na Ayubu Mhina. Pwani Mshambuliaji mpya wa mabingwa wa soka mchini Simba Sc, Adam Salamba amenusurika katika ajali mbaya ya gari baada kugongwa kwa nyuma kwa gari lake aina ya Crown alilokuwa akisafiri nalo kutokea Mwanza kurejea Dar es Salaam katika maeneo ya Vigwaza wilayani Bagamoyo mkoani Pwani. Gari la Salamba likiwa katika mwendo wa kawaida liligongwa kwa nyuma na roli kisha nalo likaenda kuigonga gari nyingine iliyokuwa mbele yake na kuifanya iharibike, hata hivyo akuhumia katika ajali hiyo kitu kilicholeta uhafadhali kwake. Mchezaji huyo alikuwa anatokea jijini Mwanza, Salamba amejiunga  na Simba akitokea Lipuli Fc ambayo nayo ilimchukua kutoka Stand United, amejiunga na Simba kwa mkataba wa miaka miwili na ameweza kucheza michuano mikubwa miwili, Sportpesa Super Cup na kombe la Kagame yote ikifanikiwa kucheza fainali