Yondani kurejea Msimbazi

Na Saida Salum. Dar es Salaam

Tetesi zilizoenea mchana wa leo jijini Dar es Salaam zinamuhusu beki kisiki wa Yanga SC ambaye amegoma kusafiri na kikosi hicho jana kuelekea nchini Kenya ambapo kesho wanaumana na Gormahia, Kelvin Yondani inasemekana anajiunga na Simba.

Taarifa ambazo mchana wa leo zilisambaa kwa kasi ni kwamba mlinzi huyo asiyechuja alionekana katikati ya jiji la Dar es Salaam zilipo ofisi za bilionea Mohamed Dewji "Mo Dewji" akiingia na kutoka huku akiwa amezungukwa na kundi kubwa la wapambe.

Mambo Uwanjani imeshuhudia Yondani akizunguka mara kadhaa na imejiridhisha kuwa kuna mazungumzo yamefanywa kati ya Simba na beki huyo ambaye mkataba wake na Yanga umemalizika.

Za udukuzi zimebaini kuwa beki huyo anaitoboa Simba shilingi milioni 50 za Kitanzania na anarejea tena nyumbani kwani kabla hajaenda Jangwani alikuwa mitaa ya Msimbazi

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FIFA yatoa orodha ya vilabu bora duniani, Simba na Yanga zachuana vikali

Beno Ngassa mdogo wa Mrisho Ngassa anayekipiga Tanzania Prisons